Dhaka: Mji uliokosa nafasi za kuzika wafu

Suraya Parveen with a photo of her father Mejbah Uddin Ahmed
Maelezo ya picha,

Suraya Parveen anasema kaburi la babake Mejbah Uddin Ahmed lilikuwa kumbukumbu ya mwisho aliyobakia nayo

Makaburi mengi mjini Dhaka, mji wenye watu wengi,ni ya muda mfupi kwa sababu, mjini Bangladesh hakuna nafasi tena ya kuzikia.Utafanya nini ikiwa mtu atachukua eneo alilozikiwa mpendwa wako?

Suraya Parveen hawezi tena kutembelea kaburi la Baba yake kwasababu mwili mwingine wa mtu asiyemfahamu umezikwa kwenye kaburi hilohilo.

''Nikiwa mtoto wa kike mkubwa,nina wajibu wa kuangalia vitu.Siku moja nilimuuliza kaka yangu kama hivi karibuni alitembelea kaburi''.Aliiambia BBC mjini Dhaka.

Baada ya kusita kwa muda, alimwambia kuwa kuna kaburi jingine jipya juu ya kaburi la marehemu baba yao.

''Familia nyingine sasa inamiliki kaburi hilo na wamekwishaliwekea sakafu.Taarifa hizi zimeniumiza sana, sikuweza kuzungumza kwa muda'' alieleza huku akibubujikwa na machozi.

Hii si mara ya kwanza tukio hili kumtokea Suraya. Kwa mtindo huohuo alipoteza makaburi mengine ya wapendwa wake,kaburi la mtoto wake wa kwanza, Mama yake na mjomba wake.

Matukio haya yamewaathiri watu wengi mjini Dhaka na kuwafanya watu kushindwa kuwa na maeneo ya kudumu ya kuwapumzisha wapendwa wao.

Si kazi ngumu kupata maeneo ya kuzika, makaburi ya muda mfupi hayana gharama, lakini sheria za mji huo zinasema kila baada ya miaka miwili,

mwili mwingine utazikwa kwenye eneo hilohilo.

Ni hali ngumu kwa watu huko lakini hawana jinsi. Wakati mwingine wanafamilia wanazikwa kwenye kaburi moja.

Kuchoma maiti haikubaliwi kwa wengi walio na imani la Kiislamu Bangladesh. Sheria za kiislamu haziruhusu kuchoma maiti katika mazishi.

Tangu 2008 maafisa wa serikali wa mji wamesitisha zoezi la kugawa makaburi ya muda mrefu, wakati karburi moja la muda mfupi waweza gharamia dola za Kimarekani elfu 20, kwenye nchi yenye mapato ya mwaka ya dola za Kimarekani 1610 kwa kila mtu.