Morgan Tsvangirai afariki dunia

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia.

Maelezo ya picha,

Morgan Tsvangirai alikuwa akitibiwa Afrika Kusini

Waziri huyo mkuu wa zamani wa Zimbabwe, 65, alikuwa akisumbuliwa na saratani na alikuwa akipata matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini. Bw Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change alikuwa akipambana kisiasa na utawala wa rais Robert Mugabe.