Syria: Watu 250 wauawa Ghouta wakiwemo watoto

Watu waendelea kufa Ghouta Mashariki wakiwemo watoto Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu waendelea kufa Ghouta Mashariki wakiwemo watoto

Idadi ya watu waliokufa katika mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na vikosi vya serikali huko huko Ghouta mashariki imefikia 250 ambapo kati ya idadi hiyo 50 wakiwa ni watoto.

Umoja wa mataifa nchini Syria umesema una mashaka makubwa juu maisha ya mamia ya raia ambao bado wapo katika eneo linalolengwa na mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali ya Syria katika eneo la Ghouta mashariki.

Mashambulizi hayo yaliyoanza siku ya jumapili bado yanaendelea na kusababisha vifo na majeruhi wengi wakiwemo watoto.

Umoja wa mataifa umeelezea mashaka yake juu ya kutokea Allepo nyingine,ambapo ukombozi wa mji huo mwaka 2016 pia ulisababisha vifo vya mamia ya raia kufuatia mashambulizi ya vikosi vya serikali.

Geert Cappelaere afisa kutoka UNICEF ameiambia BBC kuwa watoto ni miongoni mwa waliouawa

''Makundi ya watoto ni miongoni mwa watu wanauawa huko Ghouta Mashariki.watoto hawa wanalipa gharama ya uhai wao kwa jambao ambalo hawahusiki.Kama tunahitaji kuzuia umwagikaji wa damu Zaidi kwa watoto ni lazima tukubali kupata majeraha pia,na pia safari hii tunapata somo0 juu ya namna tunavyo takiwa kuwalinda watoto na kuona kwamba ni wajibu kila mmoja kuwalinda watoto.''

Idadi ya watu waliokufa ndani ya siku mbili ya mashambulizi hayo imepanda na kufikia 250 kwa mjibu wa ripoti kutoka Ghouta mashariki karibu na mji mkuu Damascus,huku kati yao 50 wakiwa ni watoto.

Mada zinazohusiana