Hawking kuzikwa karibu na kaburi la Newton na Darwin

mwanafizikia Stephene Hawking
Image caption Mwanafizikia Stephene Hawking

Nchini Uingereza taarifa imetolewa kuwa majivu ya mwanafizikia Stephene Hawking yatahifadhiwa katika eneo la Kanisa na jumba la makumbusho Westminster Abbey mjini London karibu kabisa na mabaki ya baadhi ya wanasayansi nguli waingereza, Isaac Newton na Charles Darwin.

Mkuu wa Westminster, John Hall anasema sayansi na dini vinatakiwa kufanya kazi pamoja kutafuta majibu ya maswali mazito ya siri ya maisha na Ulimwengu.

Kabla ya kufariki, Stephene Hawking alisema Sayansi haiwezi kuthibitisha kuwa Mungu hayupo, lakiniinamfanya kuwa si wa muhimu.

Katika andiko lake la mwisho, Stephene Hawking alieleza juu ya milipiko na migongano isiyokwisha ya sayari huko angani kiasi cha kila mgongano kutengeneza Ulimwengu wake.

Mada zinazohusiana