Heather Watson atupwa nje michuano ya Miami

Heather Watson atupwa nje katika michuano Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Heather Watson atupwa nje katika michuano

Mchezaji wa tenisi Heather Watson ametupwa nje ya michuano ya wazi ya Miami katika mchezo wa kwanza dhidi ya mbrazili Beatriz Haddad Maia.

Haddad Maia ameshinda kwa seti 7-6 (7-3) 6-2 na anatarajia kukutana na Zhang Shuai katika mchezo wa raundi ya pili.

Huu ni mchezo wa sita mfululizo kwa Watson kupoteza tangu afuzu hatua ya nusu fainali za michuano ya kimataifa ya Hobart mwezi Januari mwaka huu, alipoteza dhidi ya Victoria Azarenka katika mzunguko wa kwanza kwenye mchezo wa mapema michuano ya India mwezi huu.

Mada zinazohusiana