John Bolton amrithi Jenerali HR McMaster

John Bolton ateuliwa na rais Trump Haki miliki ya picha AFP
Image caption John Bolton ateuliwa na rais Trump

Rais Trump amemteua John Bolton kama mshauri wake wa masuala ya usalama wa kitaifa,kuchukua nafasi ya Jenerali HR McMaster aliyefutwa kazi.

Bwana Bolton ambaye ni waziri wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,ni mshauri wa tatu wa usalama wa kitaifa katika kipindi cha miezi kumi na nne ndani ya utawala wa Trump

John Bolton ni nani hasa?

Bolton mwenye umri wa miaka 69,amekuwa mdau mkubwa wa masuala ya sera za nje ndani ya chama cha Republican katika miongo kadhaa,na amefanya kazi katika vipindi tofauti kuanzia utawala wa Ronald Reagan, George HW Bush na George W Bush.

Rais wa Bush wa pili yeye alimteua Bolton mwakilishi wa Marekani katika umoja wa mataifa,na ndicho kipindi ambacho wanadiplomasia walimkosoa Bolton kwamba ni mtu asiye makini.

Ni mmoja wa watu muhimu waliosaidia kuibua madai ya kumiliki silaha dhidi ya Saddam Hussein aliyekuwa akituhumiwa kumiliki silaha za maangamizi.

Mada zinazohusiana