Tottenham yaiadhibu Chelsea 3-1 Epl

Tottenham yaiadhibu Chelsea

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Tottenham yaiadhibu Chelsea

Ligi kuu ya England imeendelea tena jana jumapili kwa michezo miwili Arsenal wakiwa nyumbani Emirate walifanikiwa kupata alama tatu muhimu kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya stoke city, kwa magoli ya Pire Emerick Aubameyang akifunga magoli mawili na Alexander Laccazete akifunga goli moja , nao Chelsea wakiwa nyumbani Stamford bridge walikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Tottenham.

Goli la Chelsea katika mchezo huo lilifungwa na Alovaro Morata huku Magoli ya Tottenham yakifungwa na Christian Eriksen pamoja na Delly Ally .

Wakati Chelsea ikipata kipigi hicho Meneja wake Antonio Conte amesema anaungana na familia ya Ray Wilkins nahodha wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa yupo hospitalini,Taarifa kutoka kwa mke wa Wilkins Jackie amesema mumewe ana tatizo la moyo.

Ligi hiyo ya England inatarajia kuendelea tena wikendi ijayo kwa michezo kadhaa,Everton watawakaribisha Liverpool,AFC Bournemouth ni wenyeji wa Crystal Palace, Huddersfield Town watakuwa ni wageni wa Brighton,Leceister city wenyeji wa Newcastle United ,Tottenham Hotspurs watakuwa ugenini dhidi ya Stoke city,Watford watawakaribisha Burnley,West Brom Albion watakuwa ni wenyeji wa Swansea city na Manchester City watawakaribisha Manchester United.