Zaidi ya watu 90 wauawa Douma, Syria kwa shambulio linalodhaniwa kuwa la kemikali

Picha kwenye mtandao wa kijamii, inayodaiwa kuwaonyesha watoto wakitibiwa, kutokana na madhara ya shambulio hilo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Picha kwenye mtandao wa kijamii, inayodaiwa kuwaonyesha watoto wakitibiwa, kutokana na madhara ya shambulio hilo

Rais wa Marekani Donald Trump amemkemea vikali rais wa Syria Bashar al-Assad na washirika wake Urusi na Iran juu ya shambulio linalodhaniwa kuwa ni la kikemikali, akisema kuwa kuwa "watakuwa na gharama kubwa ya kulipia shambulio hilo".

Katika msururu wa jumbe zake za Twitter, Bw Trump alimuelezea rais Assad kama "mnyama".

Serikali ya Rais Bashar Al- Assad wa Syria imekanusha kutumia kemikali hiyo ya sumu dhidi ya raia.

Mashambulio hayo yamelaaniwa vikali na Mataifa huku wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ikiunga mkono wito wa Marekani wa kufanyika kwa uchunguzi wa dharura wa mashambulio hayo na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua pale ripoti zitakapokamilika juu ya shambulio hilo.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amelaani shambulio hilo alilolisema ni njia zisizo na sababu za maangamizi.

Serikali za Syria na Urusi ambazo ni waungaji mkono wakuu wa vita eneo hilo zimekanusha kwa kejeli shutuma za kuhusika na mashambulio hayo.

Wafanyikazi wa uokoaji pamoja na madaktari walioko katika eneo la Mashariki mwa Ghouta nchini Syria, wamethibitisha kuwa yamkini zaidi ya watu 90 wamefariki katika shambulio baya la Kemikali.

Serikali ya Rais Bashar Al- Asaad wa Syria imekanusha kutumia kemikali hiyo ya sumu dhidi ya raia.

Idara ya kimataifa ya usalama nchini Marekani, inasema kuwa, inafuatilia kwa karibu mno taarifa zinazohuzunisha za matumizi ya silaha za kemikali Wilayani Ghouta Mashariki.

Taarifa hiyo inasema kwamba, maafisa wakuu wanaamini zaidi ya watu 40 waliuwawa, katika shambulio hilo-- lakini ikaongeza kuwa, idadi kamili ya waliouwawa, inaweza kuwa juu zaidi.

Utawala wa Syria umekanusha kutekeleza shambulio kama hilo.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Wanajeshi wanaounga mkono serikali ya Syria, wamekuwa wakiendelea na vita katika juhudi za kuwafurusha waasi kutoka mji wa Douma

Kundi la White Helmets, ambalo ni la utoaji msaada wa kujitolea, limechapisha picha za maiti nyingi kwenye mtandao wake wa kijamii, zikiwa ndani ya chumba kimoja kwenye ghorofa ya chini ya jumba moja, zikiwemo picha za wanawake na watoto waliofariki.

Picha hizo bado hazijathibitishwa.

Awali, ilisemekana kuwa, watu 150 waliuwawa, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.

Undani wa vita hivyo

Shambulio linaloashukiwa kuwa la kigaidi, lililolenga mji wa Douma, eneo linaloshikiliwa na waasi Mashariki mwa mji wa Ghouta, limetokea baada ya majuma kadhaa ya misururu ya milipuko ya mabomu kutoka angani, ya wanajeshi wa Syria.

Raia wapatao zaidi ya 100, wanasemekana kukwama huko, kwa pamoja na wapiganaji waasi.

Image caption Papa Francis ni mmoja wa viongozi waliolaani vikali mashambulio yanayodhaniwa kuwa ni ya kemikali ya Douma nchini Syria

Televisheni ya taifa la Syria, imelilaumu kundi kuu la Waasi la Jaish al-Islam, kwa kutia chumvi juu ya shambulio hilo, katika jaribio la lililoshindwa la kuzuia juhudi za jeshi la Syria kuendelea mbele kuwakabili.

Kumekuwa na mashambulio kadhaa ya kemikali ambayo yametokea nchini Syria, katika mapigano hayo makali yaliyodumu kipindi cha miaka 7 iliyopita.