Mshairi afungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia

Nacima Qorane in an undated handout picture from Somaliland's Human Rights Centre Haki miliki ya picha Human Rights Centre Somaliland
Image caption Poet Nacima Qorane was found guilty of bringing the state into contempt for backing Somaliland's reunification with Somalia.

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuhamasisha Somaliland kuungana na Somalia .

Makundi ya wanaharakati nchini Somaliland wamesema Bi. Nacima Qorane ameminywa haki zake za kibinadamu.

Somaliland ilijitambulisha kuwa huru mwaka 1991 licha ya kuwa taifa hilo halitambuliwi kimataifa.

Bi.Qorane alikamatwa mwezi Januari baada ya kurejea kutoka Mogadishu,mji mkuu wa Somalia ,wakati ambapo mshtakiwa alisema ametoka kuimba shairi la kuhamasisha umoja wa Somalia.

Baada ya mapigano ya mara kwa mara kaskazini magharibi mwa Somalia,hali hiyo ilisababisha mgawanyiko wa nchi hiyo na hatimaye Somaliland ikajitangaza kuwa iko huru .

Eneo hilo la Somaliland lina wakazi wapatao milioni 3.5

Mwendesha mashtaka amesema msichana huyo amepatikana na makosa ya kuitukana nchi yake na kutokuwa mzalendo wa serikali yake ya Somaliland.

Kituo cha haki za binadamu nchini Somaliland ameiomba serikali ya Somaliland kumuachia huru Nacima Qorane na kuheshimu haki za binadamu.

"Uhuru wa kujieleza ni jambo ambalo linalindwa na katiba ya Somaliland.Hivyo tumeitaka Somaliland kuheshimu katika yake yenyewe."

Mkurugenzi wa kituo hicho Guleid Ahmed Jama aliiambia BBC juu ya hofu yao kwa kukamatwa na kufungwa kwa msichana yule.

Aidha yeye sio wa kwanza kukutana na mashtaka ya namna hii kwa kuwa kuna idadi kubwa ya waandishi wa habari na wasanii waliowahi kufungwa Somaliland kwa kosa la namna hiyo hiyo.

Ifahamu Somaliland

Uhuru wa Somaliland ulipatikana mara baada ya serikali ya Somaliland kumuondoa madarakani dikteta Siad Barre mwaka 1991.

Mapigano ya kumuondoa Bwana Siad Barre ilisababisha watu elfu kumi kuuwawa na wengine kukosa makazi.

Pamoja na kwamba taifa hilo halitambuliwi kimataifa ,Somaliland imekuwa ikijitegemea na kuendesha nchi hiyo kivyake kwa upande wa siasa,ina taasisi zake ,majeshi na ina fedha yao wenyewe

Jamhuri ya Somaliland

  • Mji kuu: Hargeisa
  • Ina idadi ya watu milioni 3.5
  • Wanazugumza lugha ya Kisomali,Kiarabu na Kiingereza
  • Dini ya watu wa eneo hilo ni Uislamu

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii