Makaburi ya pamoja yagunduliwa DRC

DRC
Image caption Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamegundua makaburi matano ya pamoja mkoani Ituri,DRC

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamegundua makaburi matano ya pamoja mkoani Ituri, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba ni zaidi ya watu 260 wameuawa tangu mwezi Disemba.

Inasema kati yao 91 walikuwa wanawake.

Vikundi vya kutetea haki za kibinadamu vinakadiria watu 300,000 wamekimbia nchini DRC na kuingia nchini Uganda.

Kwa muda mrefu kumekuwa na mapigano kati ya wafugaji wa Hema na wakulima wa Lendu kuhusiana na ardhi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa waathirika wengi wamekuwa Wahema.

Mamlaka nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamekanusha uwepo wa makaburi hayo na kuzuiwa kutolewa kwa ripoti nzima.

Mada zinazohusiana