Marufuku kusafiri na wanyama Marekani

banned animal on airline Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tausi akijivinjari uwanja wa ndege, sheria mpya sasa marufuku Marekani

Kuanzia tarehe mosi mwezi wa sita mwaka huu, abiria wote wakaokuwa wanafanya safari zao na ndege za shirika la ndege la Marekani, watapigwa marufuku kusafiri na viumbe hai kama vile chura, nungunungu, mbuzi hata kama ni wanyama wa tiba.

Shurika hilo la ndege limechapisha sera zake mpya mapema wiki hii kwa kukabiliana na kuongezeka kwa wimbi la wanaharakati wa haki za wanyama wanao abiri ndege za shirika hillo huku wakichunguza watu wanaosafiri na viumbe hai .

Mbali na kupanua orodha ya viumbe vya marufuku, mtunzi pia atapaswa kuwa na kijikaratasi chenye maelezo ya daktari kwa mnyama yeyote atakayekutwa naye, endapo ni salama kuwa karibu na binaadamu .Wanyama wenye rangi za kuvutia na ngozi wazi watapigwa marufuku kusafiri kwa njia ya anga , pamoja na farasi wadogo.

Sheria mpya zinaongeza orodha ya viumbe vya marufuku kwenye usafiri anga vilinavyojumuisha wanyama kama, buibui, mbuzi, nyoka, "ndege pori", au wanyama wowote wenye harufu za kukera na wachafu .Kama hiyo haitoshi orodha bado ni ndefu viumbe hai wengine waliopigwa marufuku ni pamoja na Viumbe, vijiti, wadudu, na panya pia ni marufuku, pamoja na "wanyama wenye vidole, pembe au kwato .

Msemaji wa shirika hilo alifafanua kuwa tunajali haki za wateja wetu, kuanzia wafanya biashara na wa hadhi ya juu hadi kwa watu wenye ulemavu, na mahitaji ya halali ya huduma ya mafunzo au wanyama wa msaada, na kuongeza kuwa Kwa bahati mbaya, wanyama wasiofundishwa wanaweza kusababisha vurugu katika masuala ya usalama kwa timu yetu, wateja wetu na mbwa wanaofanya kazi kwenye ndege yetu.

Na endapo wanyama wataonyesha tabia mbaya, na mmiliki kushindwa kusahihisha, ada itadaiwa.