Rais Trump atilia shaka mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un

Rais Trump

Rais Trump ametilia shaka kufanyika mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi june huko Singapore .

Amesisitiza kuwa hata hivyo Korea kaskazini itapaswa kutimiza vigezo vilivyowekwa ambayo ni nadra kutokea.

Korea Kaskazini ilikwisha sema kuwa inaweza kujiondoa katika mkutano huo iwapo Marekani inasisitiza suala la kuachana na mpango wa silaha za nyuklia.

Rais Trump amezungumzia mkutano huo,mara baada ya kumpokea katika ikulu ya Marekani rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.

Maelezo ya picha,

Rais Kim Jong-un akiangalia mitambo ya nyukilia

Hata hivyo rais trump hakuweka wazi ni masharti gani ambayo yamewekwa kwaajili ya mkutano huo,na alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya masharti aliyiwekea Korea Kaskazini amesema kuwa suala la kuachana na silaha za nyuklia ni lazima litekekelzwe na Korea Kaskazini.

Mkutano huo kati ya rais Trump na Kim Jon-un uanatarajiwa kufanyikwa June 12 nchini Singapore ukitanguliwa na mkutano wa marais wa Korea hizi mbali uliofanyika mwezi April.

Maelezo ya picha,

Korea Kaskazini iimesema inaweza kujiondoa katika mkutano huo iwapo Marekani itasisitiza suala la kuachana na mpango wa nyuklia

Je Trump alisema nini juu ya uwezekano wa kuwepo?

Aliwaambia waandishi wa habari kuna masharti ambayo wanahitaji yatimizwe,vinginevyo mkutano hakutakuwa na mkutano.

Ameongeza kuwa mwelekeo wa Kim Jong-un umebadilika baada ya ziara yake ya pili mwezi huu nchini China.

Hata hivyo mapema hapo jana Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alielezea matumaini kuhusiana na mkutano huo akisema kuwa wapo kwenye maandalizi kuelekea mkutano huu wa June 12.

dopted a more positive position, saying the US was still working towards the 12 June date for the summit.Na aliipongeza China kwa kuweka msukumo wa kihistoria kwa Korea Kaskazini.