Lucy Bronze apata tuzo ya BBC

Lucy Bronze akifurahia mafanikio yake
Maelezo ya picha,

Lucy Bronze akifurahia mafanikio yake

Matokeo ya tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora wa Kike mwaka 2018 yametoka na mshindi ni Lucy Bronze, mwingereza anayeichezea Olympique Lyon na pia Timu ya Taifa ya England.

Maelfu ya mashabiki duniani kote hupiga kura kumchagua mshindi. Aliyemkabidhi Tuzo ni shangazi yake aitwaye Julie Touph mbele ya wachezaji wenzake wa Lyon ambao walikuwa wakimpigia makofi na kumshangilia. Pia alikuwepo mshindi wa mwaka jana Ada Hegerberg.

"Bado niko katika mshangao. Nilifurahi hata kuteuliwa tu kushiriki" Amesema Bronze ambaye aliiongoza Man City walipoipiga Birmingham City bao 4-1 na kutwaa FA Cup ya wanawake mwezi May mwaka 2017.