Vijana 12 waliokwama pangoni kwa siku 9 Thailand wapatikana hai

Picha ya vijana hao ndani ya pango Haki miliki ya picha Shutterstock
Image caption Picha ya vijana hao ndani ya pango

Video fupi imetolewa ikiwaonesha wajumbe wajumbe wa kikosi cha timu ya soka ya Thailand waliokutwa wakiwa hai ndani ya pango lililotandaa na pia lililo fura maji .

Kugunduliwa na kuokolewa kwa wavulana kumi na wawili na kocha wao mmoja wakiwa hai baada ya siku tisa za kunaswa katika pango upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Thailand kumesababisha kuwa gumzo katika vyombo mbali mbali vya habari ulimwenguni. Sauti ya kwanza kuisikia baada ya siku tisa ni ya bwana Briton John Volanthen.

Bwana Volanthen na Richard Stanton waliitwa na mamlaka za Thailand pamoja na mtaalamu wa mapangoni kutoka nchini Uingereza, Robert Harper.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Wavulana waliookolewa

Baraza la uokozi mapangoni kutoka nchini Uingereza wamearifu kuwa watatu hao waliwasili nchini Thailand siku tatu baada ya timu hiyo ya mpira kuelekea katika mapango ya Tham Luang katika mji wa Chiang Rai mahali ambako walikwenda kwenye matembezi ya kujifurahisha.

Baraza hili liliarifu kuwa mapango mengi nchini humo yanaratibiwa na wataalamu wa uokozi mapangoni kutoka nchini Uingereza, ambao hutoa uzoefu wao kutokana na kazi walizowahi kuzifanya mahali kwingine ulimwenguni.

Image caption Ramani ya kuelekea katika mapango walimonaswa vijana hao

Vijana hao wanaonekana wakiwa wamekaa katika kijisehemu cha ardhi huku wakiwa wamezunguukwa na maji, ndani kabisa ya pango mahali ambako walikwama kwa muda wa siku tisa, huku mashati yao yakiwa magotini, wavulana hao walisikika wakiomba chakula na kuondoka katika pango hilo haraka iwezekanavyo na mara juhudi za kuokozi kufanikisha zoezi hilo la uokozi, vijana hao walitoa shukrani zao za dhati.

UNESCO latangaza maeneo mapya ya kihistoria duniani

Zoezi hilo halikuwa rahisi kwa muujibu wa kikosi cha uokozi, kwani maji mara kwa mara yalikuwa yanajaa , huku tope nalo likiongeza ugumu katika zoezi hilo. Kikosi cha majini cha uokozi kutoka Uingereza ndicho kilichokuwa cha kwanza kuwasili, na hatua ya kwanza waliyofanya ni kuwatuliza kisaikolojia vijana hao kwa kuwaeleza kuwa wao ni wa kwanza kuwasili hapo na hivyo msaada zaidi unafuata.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kikosi cha uokozi

Katika mkanda wa video ulioachiliwa na kikosi cha majini cha Thailand kimewaonesha na kusikika kwa sauti mbili za kiume zinazoaminika kuwa za Waingereza hao wawilwi Wazamiaji, wakiwa na mpiga picha wa majini wakiwataka wavulana hao kuwa watulivu, huku wakiwaambia kuwa wao ndio watuwa kwanza kuwasili katika eneo hilo na kwamba watu wengi zaidi wanatarajiwa kufika eneo walipo.

Kikundi hicho cha uokozi kilipaswa kuamua mara moja kuwatoa wavulana hao kupitia katika pango hilo lililofura maji huku wakitumia zana za uokozi, ama wasubiri huku wakiwasaidia vijana hao wenye njaa na kiu ili wapate nguvu tena huku wakiondosha maji kutoka katika pango hilo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii