Trump aikosoa Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya

Rais Trump akiwa ziarani Uingereza
Image caption Rais Trump akiwa ziarani Uingereza

Rais Donald Trump amesema Uingereza huenda haitapata mikataba ya kibiashara na Marekani iwapo itaendelea mpango wake wa kwa mfumo wa sasa juu ya namna ya kujitenga na Umoja wa Ulaya.

Ameliambia gazeti la Sun kuwa mpango wa huo wa waziri mkuu utaua mipango ya kibiashara ya Uingereza na Marekani,ambapo lengo la Marekani ni kufanya biashara na Uingereza pekee bila kuhusisha umoja wa Ulaya,na ameongeza kuwa Uingereza inapaswa kutoshirikiana kabisa na umoja huo ili kuweza kuiamini na kushirikiana nayo kibiashara.

Bi.Theresa May amekuwa akijitahidi kutumia ziara hii ya kwanza ya Trump kumshawishi biahsra huru kati ya mataifa hayo mawili akisisitiza kwamba suala kujiotoa katika umoja wa Ulaya ni fursa ya kukukuza uchumi wa Marekani na Uingereza.

Katika hatua nyingine rais Trump amemsifia aliyekuwa waziri wa mambo wa nje alijiuzuru Boris Johnson na kudai kuwa anafaa hata kuwa waziri mkuu lakini wamempoteza.

Ameongeza kuwa kile kinachoendelea kwa sasa katika Uingereza kujitoa katika umoja huo wa Ulaya ni tofauti kabisa na kile kilichopigiwa kura na wananchi.

Trump amesema kuwa alimshauri Bi.May njia nzuri ya kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya lakini hakumsikiliza,hatuwezi kuwa tayari kuwa na mashirikiano ambayo ndani yake kuna umoja wa Ulaya.

Mhariri wa BBC wa masuala ya siasa Laura Kuenssberg, amesema kauli hii ya Trump inatupilia mbali madai ya Bi May ambaye amekuwa akisema Uingereza bado inaweza kuwa na makubaliano imara ya kibiashara na dunia pamoja na kuwa na ushirikiano kwa namna moja na umoja wa Ulaya.

Image caption Rais Trump akiwa na mwenyeji wake Bi Theresa May.

Naye mbunge kutoka chama cha Labour Phil Wilson, anayeunga mkono kura ya wananchi kujitoa katika umoja huo amesema maoni ya rais Trump yanaonyesha wazimpango wa waziri mkuu Bi Theresa unazidi kuonekana mbaya mbaya kila kukicha.

Leo siku ya ijumaa Bi May na Trump watakwenda makao makuu ya kijeshi kushuhudia mazoezi ya pamoja ya kikosi maalumu cha kukabiliana na ugaidi kinachoundwa na muungano wa Marekani na Uingereza.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii