Waasi wasalimu amri katika vita vya mji wa Deraa, Syria

Majengo katika mji wa Deraa yaliyoathiriwa na vita
Image caption Majengo katika mji wa Deraa yaliyoathiriwa na vita

Vikosi vya Syria vimefanikiwa kurejesha udhibiti wa mji wa Deraa, uliokuwa unashikiliwa na waasi, eneo hilo ndipo mahala alikozaliwa rais wa taifa hilo Bashar al-Assad. Waasi hao wamekubali kuweka silaha chini.

Waliingia katika eneo hilo na kufanikiwa kupandisha bendera ikiwa ni alama ya kujitangazia udhibiti wa mji huo. Waasi wamesalimu amri na kuelekea katika eneo la kaskazini ambalo ni salama kwao.

Hata hivyo majeshi hayo ya serikali pia yamefanikiwa kukamata magari ya waasi hao na mali nyingine ambazo walikuwa wakizitumia tangu walishikilie eneo hilo june 19 mwaka huu.

Umoja wa mataifa unasema kuwa watu wapatao maelfu ya raia waliokuwa wamepewa hifadhi katika mpaka wa Jordan wamerejea katika makazi yao, kufuatia waasi kusalimu amri na kukubali kuweka silaha chini hapo jana na kukubaliana na serikali.

Mji huo una umuhimu mkubwa, kwani, ni jimbo ambalo lililopo na Jordan,na ndipo zilipoanzia harakati za upinzani mwezi machi mwaka 2011.

Mada zinazohusiana