Shughuli ya uokoaji yaendelea Genoa Italia

daraja Haki miliki ya picha EPA
Image caption Daraja la mwendo kasi laanguka

Kazi ya uokoaji imeendelea kufuatia kuvunjika kwa daraja la barabara ya mwendo kasi huko kaskazini mwa Italia katika mji wa Genoa na kusababisha vifo vya watu wapatao 35.

Picha ya video inaonyesha upande mmoja wa mnara ulisababisha daraja kuanguka kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya. Sauti za kuomba msaada kutoka kwa watu wanaosadikiwa kunaswa katika mabaki ya daraja hilo zimesikika usiku kucha.

Takriban magari 30 yalianguka katika upande wa mfereji wa uchafu.

Huwezi kusikiliza tena
Tazama daraja la magari lilivyoanguka na kuuwa watu 30 Itali

Wafanyakazi wa dharura wanajaribu kuwatafuta watu walioanguka na magari yao huku wakiwa wanasaidiana na mbwa wenye utaalamu kwa kunusa .

Image caption Hali ya hewa kuwa mbaya ndio chanzo

Waziri wa usafirishaji Danilo Toninelli ameliongelea janga hilo kuwa kubwa na Ufaransa nayo imehaidi kushirikiana pamoja na Italia katika janga hilo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameandika ujumbe wa pole katika ukurasa wake wa Twitter kwa waitaliano na wafaransa pia.

Ni kwa namna gani daraja hilo lilianguka?

Image caption kazi ya uokoaji inaendelea

Majira ya saa tano na nusu (09:30 GMT) wakati wa mvua kubwa ,

''Polisi iliripoti juu ya mvua kubwa iliyokuwa inanyesha muda huohuo ndio nilipoona mwanga ukimulika katika daraja na mara daraja likaanza kushuka chini",shahidi alieleza

Shahidi mwingine alisema kwamba tulisikia muungurumo mkubwa na mwanzoni tulidhani kuwa ni radi ambayo iko karibu nao.

Naibu waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo ,Edoardo Rixi amesema idadi ya vifo ni 35 lakini wanatarajia kuwa vifo hivyo vinaweza kuongezeka.

Image caption Ramani ikionesha jinsi daraja hilo lilivyoanguka

Daraja hilo ambalo lilijengwa tangu mwaka 1960,lilikuwa linawahudumia waitaliano na wafaransa ni miongoni mwa madaraja kumi nchini humo.

Serikali ya Italia hivi karibuni ilihaidi kuongeza kiwango cha uwekezaji katika miundombinu .

Mwaka 2006 taifa hilo lilitumia zaidi ya yuro bilioni 14 kwa ajili ya matengenezo ya barabara lakini mwaka 2010 kiasi hicho cha fedha kilipungua yuro bilioni nne kwa mujibu wa shirikisho la uchumi na maendeleo ( Economic Co-operation and Development).

Mada zinazohusiana