Bobi Wine kufikishwa mahakama ya kijeshi leo Uganda

Bobi Wine akiwa na wafuasi wake

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Bobi Wine akiwa na wafuasi wake

Mbunge ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Wakati huo huo Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu wanahabari.

Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

zaidi ya wasanii 80 wanataka Bobi wine aachiwe Huru akiwemo Chris Martin (kustoto), Angelique Kidjo (katikati) na Damon Albarn (kulia)

Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wanakataa kumtesa.

Anatarijiwa kufikishwa mahakamani juu ya madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria.

Waraka huo umeanzishwa na Rikki stain aliekua msimamizi wa zamani wa mawamuziki fella kuti ambae alikua mkosoaji mkubwa wa serikali ya Nigeria

Anasema kuwa likua akipigwa hata kwa kuzungumza.

Zaidi ya watu 80 akiwemo mwandishi mkongwe whole soyinka na wanamuziki wa kundi la U2 bassist Adam Clayton, muambiaji kiongozi Chrissie Hynde na Genesis Peter Gabriel.

Jeshi ambalo ndilo linamzuia Wine linasema kuwa hajateswa na Rais Yoweri Museveni ametupilia mbali madai hayo na kuzitaja kuwa habari za uongo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Bobi Wine

Bobi Wine ni nani?

Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.

Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.

Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).

Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.

"Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki...Ninataka siasa zitulete pamoja... jinsi muziki ufanyavyo."