Mkurugenzi mkuu CBS Les Moonves akumbwa na kashfa ya ukatili wa kingono

Chanzo cha picha, AFP
Mkurugenzi mkuu wa CBS Les Moonves ajiuzuru
Mkuu wa shirika la habari maarufu nchini Marekani la CBS Les Moonves,amejiuzuru kutokana na kukumbwa na kashfa ya ukatili wa kingono.
CBS kwa muda mrefu wamekuwa wakimchunguza Moonves tangu zitokee kashfa hizo mjini New Yorker mwezi July na madai mapya dhidi yake yaliyotokea siku ya jumapili dhidi ya wanawake wengine sita.
Moonves, mwenye umri wa 68,amekanusha madai hayo na kudai kuwa ni mambo ya kushangaza.
Hata hivyo shirika la CBS limesema kwa kushirikiana na Moonves wanachangia kiasi cha dola million 100 kwa makundi yanayounga mkono harakati ijulikanayo kama #MeToo movement.
Kauli iliyotolewa na shirika hilo inasema kuwa Moonves anatakiwa kuachia madaraka kama mwenyekiti,rais na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo haraka iwezekanavyo, ambapo kutokana na kujiuzuru huko Joseph Ianniello kwa sasa atahudumu kama kaimu mkurugenzi mkuu.
Chanzo cha picha, AFP
Gazeti la Financial Times linasema kuwa Moonves amejiuzuru kwa kuwa alijua kwamba atatakiwa kulipa fidia nzito ya hadi kiasi cha dola million 100 kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Marekani.
CBS pia wanasema kuwa hatapata mafao yoyote hadi pale matokeo ya uchunguzi huru yatakapo tolewa kuhusiana na ukiukwaji wa maadili dhidi yake.
Moonves sehemu ya mafao yake itakatwa ili kuchangia makundi yanayoendesha usawa kwa wanawake mahala pa kazi.
Kwa upande wake Moonves amekaririwa akikanusha vikali madai hayo na kwamba si ya kweli,lakini amekiri kwamba alikuwa na mahusiano ya makubaliano na wanawake watatu miaka 25 iliyopita.