Marekani yafunga ofisi za PLO Washington

Ofisi za PLO mjini Washington nchini Marekani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ofisi za PLO mjini Washington nchini Marekani

Marekani imeamuru kufungwa kwa ofisi za shirika la harakati za ukombozi wa Palestine zilizopo mjini Washington,kwa madai kuwa taifa hilo haliungi mkono mazungumzo ya Amani ya Israel.

Hata hivyo idara za Marekani zimeitaja Plaestina kwamba ilijaribu kuhamasisha mahakama ya kimataifa ya ICC kufanya uchunguzi dhidi ya Israel.

Kiongozi mwandamizi wa PLO Hannan Ashrawi, amesema Marekani inapotosha kwani hakuna mazungumzo ya Amani wala mpango wa mazungumzo hayo.

"Marekani imeamua binafsi kuutoa mji wa Israel kwa Israel,jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwa sababu Jerusalemu ni eneo lililo chini ya utawala na ni ardhi ya Palestina''. Hannan Ashrawi

Wameamua binafsi,kusababisha shida kwa wakimbizi wa Palestina na kusitisha misaada ya kifedha kutoka UNWRA ambalo ni shirika la kimataifa maalumu kwaajili ya kulinda na kusaidia wakimbizi wa Wapalestina.

Watoto laki tano kufa kwa njaa mwaka huu: Save the Children

Kuharibika mimba kilio cha wanawake

Hivyo ni unafiki kutaja suala la mazungumzo ya Amani.Na kwa sasa tunaadhibiwa kwa sababu tulitaka Mahakama ya kimataifa ya ICC kuongeza kasi katika uchunguzi dhidi ya uhalifu wa kivita unaofanywa na Israel. Kama unavyojua kwamba suala la ukiukwaji wa kimakazi ni uhalifu wa kivita kwa mujibu wa makubaliano ya Rome.")

Hatua ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalemu na kuitambua Jerusalemu kama eneo la Israel ni jambo ambalo limezusha mjadala na kuongeza uhasama kati ya Israel na Plestina.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii