Polisi nchini Kenya waendelea kumtafuta Mwitaliano Silvia Romano baada ya kutekwa Kilifi

Kenya ,Silvia Roman atekwa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wenye silaha walishambulia makazi ya Silvia Romano siku ya jumanne wiki iliyopita

Polisi nchini Kenya imetangaza zawadi nono ya dola za kimarekani milioni kumi sawa na fedha za kitanzania milioni ishirini na tatu unusu kama zawadi kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mfanyakazi wa misaada mwenye asilia ya Italia na kuwakamata wanaume watatu wanaoshukiwa kumteka jumanne iliyopita.

Silvia Romano, mwenye umri wa miaka 23 alitekwa na watu wenye silaha akiwa katika hoteli ya mtaani katika kata ya Kilifi kusini-mashariki mwa nchi hiyo.

Watu watano, wakiwemo watoto watatu, walijeruhiwa katika shambulio hilo la kumteka Silvia na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Polisi imearifu kuwa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha Silvia anapatikana na watekaji wake wabatiwa nguvuni.

Bado haijafahamika wazi sababu za kutekwa kwa mfanyakazi huyo wa kujitolea, aliyetekwa na wahuni wa mtaani endapo watekaji hao watataka kikombozi ili kumuachilia mateka wao ama lah! Ama pengine inakisiwa watekaji wanaweza kuwa na uhusiano na wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabab.

Image caption Ramani ya eneo alikotekwa mfanyakazi huyo wa mashirika ya misaada

Polisi tayari wamekwisha sambaza picha ya washukiwa watatu katika mtandao wa kijamii wa twitter, wakielezea namna watu hao walivyo kwamba "wenye silaha na hatari".

Mpaka sasa watu ishirini wamekwisha kamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo, nalo shirika la habari la AFP wanaarifu wakimnukuu mkuu wa jeshi la polisi nchini Kenya Joseph Boinett.

Historia ya utekaji

bi Romano,alikuwa ni mfanyakazi wa kujitolea katika shirika la Kiitalino la Africa Milele Onlus, ambaye ni mfanya kazi wa kwanza kutoka katika shirika la kigeni kutekwa nchini Kenya tangu nchi hiyo kukumbwa na kipindi cha mpito cha matuko ya utekaji nyara yaliyokuwa yamekithiri na kutishia sekta ya utalii kuporomoka mnamo mwaka 2011.

Mpaka sasa kundi wa wanamgambo wa kigaidi la Al-Shabab linashukiwa kuwa mtekelezaji wa mauaji ya mwanaume mwenye asili ya Uingereza na kumteka mke wake kutoka katika kisiwa cha mapumziko mnamo mwaka 2011.

Wiki kadhaa baadaye, mwanamke mwenye ulemavu wa asili ya Ufaransa alipochukuliwa kutoka nyumbani kwake katika visiwa vya mji wa Lamu na kuarifiwa baadaye kuwa amefariki dunia wakati akiwa mateka.

Wafanyakazi wa kujitolewa wawili wenye asili ya Hispania nao walitekwa mwaka huo huo wa 2011 na watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kijihadi kutoka katika kambi ya Dadaab ambayo iko karibu na mpaka wa nchi ya Somalia.Na kuarifiwa kuwa waliachiliwa miezi ishirini na mmoja baadaye.

Mada zinazohusiana