Rais Muhammadu Buhari aizuru Maiduguri

Majeshiya Nigeria na ziara ya raisi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption ais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amewasili kwa ziara ya siku moja ya kikazi maeneo ya Maiduguri, mji mkuu ulioko jimbo la Borno na ndiko mahali ambako limezaliwa kundi la wanamgambo wa kiislamu Boko Haram.

Akiwahutubia askari waliopelekwa mstari wa mbele katika vita vya kupambana na jeshi la wanamgambo wa Boko Haram ambao bado wanaendesha harakatin zao za kutisha maeneo makubwa ya kaskazini-mashariki mwa nchi ya Nigeria.

Ziara yake imekuja siku chache tu baada ya shambulio la kambi ya kijeshi iliyoko Metele, shambulio ambalo limekuwa matokeo ya vifo vya wanajeshi arobaini.Rais Buhari amevitembelea vikundi vya wanajeshi waliojeruhiwa ambao bado wanaendelea na matibabu katika kituo cha kijeshi mjini Maiduguri.

Image caption Rais Buhari awatembelea wamajeshi walioko mstari wa mbele

Serikali ya Buhari na jeshi lake imekuwa ikipingwa tangu mashambulizi hayo, jeshi nchini humo limechukua siku tano kuweza kuthibitisha juu ya shambulizi hilo na kupinga juu ya vifo vya wanajeshi wenzao.

Image caption wanajeshi wakana kuuawa kwa wenzao nchini Nigeria

RaisI Buhari, anakabiliwa na uchaguzi mnamommwezi wa pili mwaka , na ameingia madarakani mnamo mwaka 2015 na wakati wa kampeni zake aliahidi kupambana na makundi ya kigaidi nchini mwake, ambaye amekuwa akinukuliwa mara kwa mara kuwa amefanikiwa kuyashinda makundi hayo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, alinukuliwa akisema kuwa angeweza kuvuka "vikwazo" vya ugaidi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii