Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 06.12.2018: Hazard, Fekir, Cavani, De Jong, Nakajima, Heaton, Mutch

Eden Hazard Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard alijiunga na Chelsea mwezi Juni 2012

Real Madrid imefikia makubaliano ya kibinafsi na Chelsea kuhusiana na usajili wa kingo mahiri Hazard,27, msumu huu wa joto. (Onda Madrid, via AS)

Wolves wanapania kumsajili winga wa Japan Shoya Nakajima kutoka Portimonense ya Ureno mwezi Januari, huku Leicester na Southampton nao wakimmezea mate winga huyo wa miaka 24. (Mail)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anatafakari uhamisho wa mshambuliaji Wesley Moraes kwa kima cha euro milioni 15, japo Fiorentina na Valencia pia zinamfuatilia kiungo huyo wa Brazil . (Sun)

Aston Villa wanapigiwa upatu kumsajili kipa wa Burnley na England Tom Heaton, ambaye ni chaguo la tatu katika uga wa Turf Moor. (Mirror)

Meneja wa Leeds Marcelo Bielsa amepuuzilia mbali tetesi kuhusiana na uwezekano wa kuwamsajili makipa Tom Heaton, 32, wa Burnley na Freddie Woodman, 21, wa Newcastle kwani yuko mbioni kumtafuta kipa mpya. (Mirror)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tom Heaton, kipa wa Burnley

Cardiff wanapanga kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Jordon Mutch.(Sun)

Mmiliki wa Lyon Jean-Michel Aulas anataka kushughulikia hatima ya mshambuliaji wa Ufaransa Nabil Fekir kufikia sherehe ya krismasi. Pendekezo la kiungo huyo la kuhamia Liverpool msimu wa joto liligonga mwamba. (Le Progres - in French)

Meneja mpya wa Jamhuri ya Ireland Mick McCarthy atajaribu kumshawishi kiungo w kati wa West Ham Declan Rice, 19, asibadili msimamo wake na kuelekea Uingereza. (Telegraph)

Kipa wa Paris St-Germain Gianluigi Buffon amesema haoni uwezekano wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 31, kurejea Napoli mwezi Januari. (Tiki Taka, via FourFourTwo)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa PSG Neymar (kushoto) na Kylian Mbappe(kulia)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe anasema Frenkie de Jong, 21, ambaye ni kiungo wa kati wa klabu ya Ajax na timu ya taifa ya Uholanzi atakaribishwa kwa mikono miwiliPSG. (France Football)

Inter Milan huenda ikajaribu kumsajili beki wa kupanda na kushuka wa Manchester United na Italia Matteo Darmian mwakani, baada ya kushindwa kuchukua kiungo huyo kwa mkopo msimu uliyopita. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Meneja mpya wa Real Madrid boss Santiago Solari amesema uamuzi wa iwapo klabu hiyo uwasajili wachezaji wapya mwezi Januari si wake. (Marca)

Sasa imeibuka kuwa huenda Arsenal iliamua kumuajiri Unai Emery kuchukua nafasi ya Arsene Wenger badala ya Mikel Arteta kwa sababu aliwasifia wachezaji wa klabu hiyo na kwamba hakutaka kufanya mabadiliko makubwa. (Telegraph - subscription required)

Baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza msimu huu, Gunners hawajashindwa katika mechi 20 sasa chini ya Emery.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Unai Emery(kulia), meneja wa Arsenal

Tetesi bora ya Jumanne

Kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 25, amesema haoni sababu ya kujiunga na Paris St-Germain mwezi Januari mwakani licha tetesi kuwa huenda akahamia klabu hiyo ya Ufaransa. (UOL, via FourFourTwo)

Juventus wanatafakari kuweka dau la kumnunua Paul Pogba,25, kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Fabinho Kiungo wa kati wa Liverpool

Everton sasa inapania kutumia uamuzi wa kiungo huyo wa miaka 25 kuimarisha dau lake kwa lengo la kupampatia mkataba wa kudumu. (Times)

Kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes anayechezea klabu ya Everton kwa mkopo hajaonesha nia ya kutaka kurudi Barcelona.

Mshambuliaji wa LA Galaxy na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 37, huenda akarejea AC Milan hivi karibuni bada ya mazungumzo kuhusiana na mpango huo kushika kasi.(Goal)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii