West Ham kuchunguzi matusi ya ubaguzi dhidi ya mshambuliaji wa Liverpool Salah

sports Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mohamed Salah akabiliana na ubaguzi wa kidini michezoni

Timu ya West Ham inachunguza tukio la baada ya video iliyo tandaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha shabiki mmoja akimshambulia, mshambuliaji wa timu ya Liverpool Mohamed Salah wakati wa mchezo uliochezwa mwanzoni mwa wiki , mchezo uliozaa sare ya bao moja moja kwenye uwanja wa London uliopigwa mwanzoni mwa wiki hii.

Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Misri Salah, mwenye umri wa miaka 26, alirekodiwa kwenye kipande cha video kwa njia ya simu upande walikokuwa wamekaa washabiki wa timu yake katika uwanja wa nyumbani wakati alipokuwa akijiandaa kuupiga mpira wa kona.

Kipnde hicho cha video, kilirekodiwa na shabiki wake, ikinaonesha akitupiwa maneno makali ikiwemo yake ya kiislam.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Mohamed Salah

Katika taarifa yake, timu hiyo ya West Ham imearifu kuwa wao kama timu "wana sera ya kuvumiliana kwa kiwango kikubwa kwa aina yoyote ya tabia ya vurugu au ya mateso".na kuendelea kueleza kuwa Sisi ni klabu ya soka inayojumuisha.

Mtu yeyote anayejulikana kufanya kosa atatakiwa kutoa maelezo kwa polisi na atakabiliwa na marufuku maisha ya kutoingia kushuhudia mtanange wa timu hiyo na timu zingine katika viwanja hivyo vya London, hakuna nafasi ya tabia kama hizo katika viwanja vyetu .

Mtu aliyerekodi kipande hicho, baadaye alikiweka katika mtandao wa twitter akieleza kuwa "Nilikuwa na wasiwasi na kile nilichosikia. Watu kama hawa hawastahili nafasi yoyote katika jamii yetu achilia mbali mchezo wa mpira wa miguu ."

Inaarifiwa katika taarifa ya klabu hiyo kuwa shambulio hilo la maneno limeshafikishwa polisi''Tunastaajabishwa kuona tukio lingine la hali ya juu la ubaguzi katika soka la Uingereza.

  1. Salah atawazwa mchezaji bora wa mwaka wa CAF
  2. Je ni kweli Mohamed Salah anakabiliwa na ukame wa mabao?
  3. Mo Salah: Ilikuwaje akawa mchezaji nyota?
Haki miliki ya picha iStock
Image caption uwanja wa London

Polisi nchini Uingereza walitoa taarifa yao , "Tunafurahi kuwa viongozi wa West Ham wameonyesha uamuzi wao na kumtambua mbaguzi huyo na kuchukua hatua imara na kwamba aina hii ya tabia haikubaliki na inapaswa kuwa changamoto kwa haraka na kwa uamuzi. "

Ikumbukwe kwamba Salah, anatajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa kombe la shirikisho PFA nchini humo, Mchezaji , Mwandishi wa Soka wa Mwaka na Mchezaji wa Ligi Kuu ya Mwaka msimu kwa mwaka wa jana baada ya mabao yake 32 aliyotingisha nyavu na kuweka rekodi mpya kwa zaidi katika msimu wa michezo 38.

Amekuwa akimwagiwa mvua ya sifa na Steve Rotheram,ambaye ni meya wa mji wa Liverpool, kwa kusaidia kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na "kuvuka vikwazo vya namna hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwa mfano wa kuigwa miongoni mwa watoto Kiislam.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii