Tembo mzee zaidi duniani afariki dunia

tembo mzee afariki Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dakshayani, pichani mnamo mwaka 2016, alikuwa akiishi aliishi Hekalu la Chengallur Mahadeva kusini mwa Kerala

Dakshayani, anayefikiriwa kuwa tembo wa zamani kabisa duniani, amekufa akiwa na umri wa miaka 88 nchini India.

Kutokana na kichwa cha gaja Muthassi au kijana wa tembo, Dakshayani alishiriki katika ibada za hekalu na maandamano katika Hekalu la Chengalloor Mahadeva katika jimbo la kusini la Kerala.

Lakini mtunzaji na mwenye kumtibu tembo huyo alionekana naye mapema wiki hii akiwa amesimama naye huku akimpa chakula na inasemekana tembo huyo mzee alikufa Jumanne.

Wahifadhi wa tembo huyo walianza kumlisha mananasi na karoti miaka ya hivi karibuni baada ya kukabiliwa na tatizo la kushindwa huku na kule na kushindwa kuonekana hadharani na katika shughuli za kijamii kwa miaka kadhaa sasa.

Bodi ya Travancore Devaswom, ambayo inaendesha hekalu ambalo alikuwa akiishi tembo mzee, inaarifu kuwa tembo huyo ni wa zamani kabisa katika uhamisho na anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 88.Hata hivyo, mmiliki wa sasa wa Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa tembo wa zamani katika utumwa ni Lin Wang.

  1. Mtalii auawa baada ya kukanyagwa na Tembo
  2. Tembo anayetoa 'moshi' mdomoni India
  3. Kampuni ya China yawanusuru tembo wanne Tanzania

Tembo wa bara Asia alikufa kwenye bustani ya wanyama huko Taiwan mwaka 2003 akiwa mimwenye umri wa miaka 86, na kutumikia na wasifu wake uinaarifu kuwa kipindi cha uhai wake aliwahi kulitumikia Jeshi la Uingereza katika Vita Kuu vya Pili vya dunia.

Ndovu mwingine ni Indira, alikufa nchini India katika jimbo la Karnataka mnamo mwaka 2017 na iliripotiwa kuwa alikuwa mzee wa "kati ya miaka 85 ama 90".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tembo alishirikishwa katika ibada za hekaluni na maandamano pia

India inakadiriwa kuwa na idadi ya tembo elfu mbili na mia nne walioko uhamishoni, Rais wa zamani wa Bodi ya Travancore Devaswom aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Dakshayani alikuwa akitunzwa vizuri .

Rais wa zamani wa Bodi alinukuliwa akisema kuwa ''Kutokana na vikwazo mbalimbali vya vitendo vya jamii, hatukuweza kumuachilia huru, lakini badala yake akahakikisha kwamba alikuwa na nafasi ya kutosha kuzunguka," alisema.

Maisha ya kutisha ya tembo kuwekwa mateka nchini India ili kuwasaidia watalii kuwaona kirahisi ingawa kwa upande mwingine hali hiyo inazidi 'kuchochea ukatili' dhidi ya wanyama hao.Hata hivyo watetezi wa sayansi wanasema tembo wengi wanakabiliwa na hali mbaya.