Mkenya shutumiwa kimakosa kwa maambukizi hatari ya zinaa
Huwezi kusikiliza tena

Picha ya saratani ya uume wa George ilisambaa mtandaoni na kutumiwa katika taarifa feki

Hebu fikiria picha ya sehemu zako za siri kutumiwa kinyume na matakwa yako huku ukionyeshwa hospitali ukiwa nusu uchi kwenye mitandao ya kijamii. Hivi ndivyo taarifa za vyombo vya zilivyoenezwa zikielezea kile kilichosemekana kuwa ni ugonjwa mpya hatari unaoenezwa kwa zinaa uitwao Jakadala. Mwandishi wa BBC Ian Wafula amekuwa magharibi kwa kenya na kuzungumza na mwanaume ambaye picha yake ilisambaa mitandaoni. Hata hivyo taarifa yake imekuwa na manufaa kuliko unavyodhani.