Baraka Shenouda fundi cherehani anayeshona kwa miguu

Baraka Shenouda fundi cherehani anayeshona kwa miguu

Baraka Shenouda alizaliwa bila mikono miaka 30 iliyopita nchini Misri.

Lakini anasema hilo halijamzuia kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine walio na mikono.

Amejizolea sifa ya kuwa fundi cherehani stadi anayeshona nguo kwa kutumia miguu yake.

Sheria mpya iliyoidhinishwa hivi karibuni nchini Misri inatarajiwa kutoa nafasi nyingi za kazi kwa watu walemavu.

Baraka anajifunza kusoma na kuandika ili siku moja apate ajira na kushi maisha mazuri zaidi.