Kwanini wanawake Burundi hawaja thubutu kufanya kazi ya uvuvi?

Uvuvi Burundi

Wanawake wengi nchini Burundi wangependelea kuwa wavuvi,Lakini hawaja thubutu kufanya kazi hiyo kutokana na na vikwazo vya kitamaduni.

Kazi ya uvuvi , imedhihirika nchini burundi sawa na nchi nyengine duniani kuwa ni wanaume tu ndiyo wanaifanya

Mila za kumkataza mwana mke kuingia majini na kuvua samaki zimetokana na nini?

BBC imefanya utafiti na kuzungumza na baadhi ya wavuvi wa kwenye ziwa Tanganyika , na baadhi ya wanawake wanao fanya biashara ya samaki karibu na kivuko cha kajaga.

Mmoja wa wanawake hao ni Yolanda Hakizimana mwenye umri wa miaka 37,ambaye amejitokeza wazi kuelezea jinsi wanawake wanavyotengwa katika kazi hiyo ya uvuvi.

''Wanaume wavuvi husema mwanamke akiingia katika mtumbwi basi samaki wote majini wana tawanyika'' alisema.

Wengine wanasema kuwa mwanamke akiwa katika hedhi au akiwa na mimba changa basi haruhusiwi kukaribia eneo la ziwa.

Yolanda anayapuuza madai hayo na kusema kuwa ni dhana iliyopitwa na wakati na kwamba ni ukosefu wa kutojua wa wanaume.

''Inasikitisha kusikia wanaume wanadai mwanamke akingia majini kwa uvuvi samaki wanakimbia na kutawanyika''

''Sisi tunasafiri kila mara katika mitumbwi kwenda DRC, mbona hakuna hasara ao ajali yoyote imewahi kutokea ?'' anauliza Yolanda.

Ameongeza kuwa wakati umewadia na wanawake pia kufanya kazi ya uvuvi bila masharti.

Bi Yolanda pia anapendekeza wanawake waruhusiwe kujiunga katika mashirika ya uvuvi kwa wanawake.

Wanaume wengi kwenye eneo la ziwa Tanganyika wanapinga kauli hiyo na wanashikilia kuwa wanawake hawawezi kabisa kuwa wavuvi.

Wanadai kuwa masuala ya hedhi na uja uzito yanaashiria udhaifu wa mwanamke.

Lakini wataalaamu wa masuala ya ki jamii wanasema nini ?

Professa Emile Mworoha, ambaye ni pia ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Burundi na mtaalam wa masuala ya Historia anasema kihistoria jamii ya Warundi imezungukwa na mila zinazo kataza mambo kadha wa kadha.

Kazi ya uvuvi ni kazi ngumu sana kwa sababu inafanyika usiku, watu wengi wanahoji ikiwa mwanamke una kufanya kazi hiyo akiwa na mtoto mgongoni.

"Ni tatizo kubwa haitoshi ukitathmini mila na desturi za Burundi unakuta mambo mengi yamekatazwa'' anasema Profesa Mworoho.

Katika mila za kirundi, mwanamke haruhusiwi kupanda juu ya nyumba na kujenga dari, au afanye kazi ya kuuza nyama katia buchari au sokoni.

Pamoja na hayo yote katika sekta nyinginezo mwanamke wa Burundi anashiriki katika kazi mbali mbali zinazo hitaji nguvu nyingi kama vile kuhudumu jeshini, polisi, au hata ujenzi wa barabara.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii