Watu zaidi ya 50 wamefariki dunia katika ajali Ghana

Basi lililoungua moto kwenye eneo la ajali

Chanzo cha picha, Anas Sabit-Kask

Maelezo ya picha,

Wengi miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye mabasi yote mawili walikufa hapo hapo

Mtu mmoja amekuwa akimshirikisha mwandishi wa BBC nchini Ghana picha kutoka eneo la ilipotokea ajali lililopo katika mji wa Kitampo uliopo katikati mwa nchi hiyo Ghana, ambako watu zaidi 50 wamekufa baada ya mabasi mawili kugongana mapema Ijumaa.

na bado wa hawajaokolewa.

Polisi wanasema basi ziliwaka moto.

" Wengi miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye mabasi yote mawili walikufa hapo hapo.

Chanzo cha picha, Anas Sabit-Kaskiya

Maelezo ya picha,

Polisi wanasema huduma za zima moto kwa sasa zimefika eneo la ajali

Baadhi yao waliokuwa na majeraha walikimbizwa hospitalini ," alisema msemaji wa polisi.

Baadhi walikwama katika mabadi hayo mawili

Polisi wanasema huduma za zima moto kwa sasa zimefika eneo la ajali.

Tutakufahamisha zaidi kuhusu taarifa hii kadri tunavyozipata.