Wapenzi wa jinsia moja matatani Brunei
Huwezi kusikiliza tena

Je hatua ya kutetea wapenzi wa jinsia moja imefeli Brunei?

Tangu Brunei iilipotangaza itaanza kutekeleza sheria kali ya kiislam ya kupigwa mawe kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi ya mahusiano ya watu wa jinsia moja ,wasanii wengi wa kimataifa wameanzisha kampeni ya kupinga hatua hiyo.

Wasanii hao ni wale wa huko Ulaya kama akina Elton na Ellen. Na sasa Will Clooney's nae atoa wito kususiwa kwa mahoteli ya kifahari ya nchi hiyo ya kifalme, ambayo ni ndogo lakini tajiri sana.

Hata hivyo Sultan wa Brunei Hassanal Bolkiah ni kama hatingiki, Asema "Ninataka mafunzo ya kiislamu yakiwa thabiti Brunei," Je kampeni hiyo imegonga mwamba? Sema nasi kupitia ukurasa wetu wa facebook, BBC SWAHILI.COM