Tanzania: Mchungaji kutoka Nigeria akabiliwa na tuhuma za dawa za kulevya

dawa

Raia watatu wa kigeni akiwemo anayejiita mchungaji kutoka nchini Nigeria Hemry Ozoemena Ugwuanyi wananaswa na kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya cha nchini Tanzania wakiwa na kilo 15 za dawa za Heroine.

Hatua hii ya mchungaji huyu kunaswa akiwa na dawa za kulevya ni gumzo katika makundi mbali mbali nchini humo na hasa ukizingatia hadhi na uaminifu mkubwa ambao wamekuwa wakipewa wachungaji na makaasisi.

Maelezo ya video,

Sumu ya panya yageuzwa dawa za kulevya Tanzania

Mchungaji huyo alikamatwa mara baada ya raia mwingine wa kigeni nchini humo kukamatwa katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa kuwa mchungaji Hemry Ozoemena Ugwuanyi ndiye aliyempa mzigo wa dawa za kulevya kusafirisha kwenda Poland.

Huu ni mwaka wa tatu tangu mchungaji huyo aanze kufanya shughuli zake za uchungaji nchini Tanzania.

Lakini je, wachungaji nchini humo wana maoni gani ?

Mchungaji Raphael Kitime ni mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemblis of God anasema yanayotokea yanaharibu huduma ya kichungaji lakini hata maandiko yako wazi kuwa watu wajihadhari na manabii wa uongo.

Cha msingi ni serikali kuwa makini katika kusajili haya makanisa na wanaoumia ni raia.

Hao watu ni manabii wa uongo na wanataka kuwaumiza raia na kuwaibia fedha zao hivyo hata jamii wanapaswa kuwa makini zaidi.

Edwin Soko ni mwanaharakati wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya."Hali hii ya makundi maalum kujihusisha na tuhuma hizi za kukamatwa na dawa za dawa za kulevya inasikitisha sana.

Vita dhidi ya dawa za kulevya haina mwenyewe, na upana wake n mkubwa, Sheria ipo lakini tushirikiane" Erick asisitiza.