Mzozo wa Sudan: Jeshi na upinzani waaafikiana juu ya kipindi cha mpito cha miaka 3

Waandamanaji wa Sudan wakipeperusha mabango wakati wa maandamano mjini Khartoum Mae 14, 2019 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Madai ya waandamanaji ya kuwepo kwa utawala kamili kwa raia yamekuwa yakiendelea

Viongozi wa kijeshi wa Sudan wametangaza makubaliani na muungano wa upinzani juu ya kipindi cha mpito cha miaka mitatu kwa ajili ya kuukabidhi utawala wa kiraia.

baraza la kijeshi la mpito (TMC) limesema kuwa muungano utakuwa na theruthi mbili ya viti katika baraza la bunge.

Sudanimekuwa ikitawaliwa na baraza la jeshi ltangu mwezi uliopita baada ya mapinduzi ya rais Omar al-Bashir.

Maandamano yaliyosababisha kuanguka kwa utawala wake yamekuwa yakiendelea huku waandamanaji wakidai kuwekwa kwa serikali kamili ya kiraia.

Saa kadhaa kabla ya mkataba wa sasa kutangazwa, takriban waandamamnaji watano na afisa mmoja wa usalama walikufa katika makabilianokatika mji mkuu Khartoum.

Nini hasa walichokubaliana?

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Luteni Jenerali Yasser al-Atta alisema kuwa makubaliano ya mwisho juu ya mgawanyo wa madaraka yatasainiwa pamoja na upinzani - Azimio la the Declaration of Freedom na Change Forces (DFCF) - katika kipindi cha saa 24. makubaliano hayo yatajumuisha kubuniwa kwa baraza la kujitawala ambalo litaongoza taifa mpaka uchaguzi utakapofanyika.

"Tunaapa kwa watu wetu kwamba makubaliano yatakuwa yamekamilika katika kipindi cha saa 24 kwa njia inayotarajiwa na watu," alisema.

Jenerali Atta amesema kuwa DFCF utakuwa na theruthi mbili ya viti 300 vya bunge la mpito huku viti vilivyosalia vikichukuliwa na vyama ambavyo si sehemu ya muungano wa upinzani

Awali, msemaji wa vuguvugu la waandamanaji Taha Osman alisema kuwa pande zote zimekubaliana juu ya muundo wa mamlaka zijazo za utawala - baraza la utawala , bunge na baraza la mawaziri

Mjumbe wa DFCF Satea al-Hajj alielezea matumaini yake kuwa yaliyomo kwenye mkataba wa mwisho juu ya mgawanyo wa madaraka yatakubaliwa : "Maoni yamekubalika na kwa mapenzi ya Mungu, tutafikia makubaliano karibuni ."

Haki miliki ya picha Getty Images

Awali jeshi lilitaka kipindi cha mpoito cha miaka miwili huku kiongozi wa waandamanaji alitaka kipindi cha mpito kiwe cha miaka minne.

Hali hii imefikaje hapo?

Mwezi Desemba , waandamanaji walianza kuandamana dhidi ya maamuzi ya serikali katika mgawanyiko wa uongozi mara baada ya rais aliyeongoza miaka 30 kuondolewa madarakani.

Katika wiki tano za maandamano , tarehe 17 Januari, watu walioshihudia kikosi cha usalama wakirusha bomu la machozi na kusababisha mauaji ya daktari.

Daktari huyo ambaye alikuwa anatibu watu waliojeruhiwa katika maandamano nyumbani kwake Khartoum , wakati ambao polisi walirusha bomu la machozi katika jengo lake. ,

Shuhuda aliiambia BBC kuwa daktari ni miongoni mwa watu wengi waliouwawa wakati ambapo waandamanaji walikuwa wanapinga serikali.

Baraza la uongozi wa jeshi lilichukua utawala tangu April 11 lakini waandamanaji walisisitiza uongozi ukabidhiwe kwa raia jambo ambalo lilikuwa linapingwa na utawala wa kijeshi.

Unaweza pia lkutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Picha hii inaashiria nafasi ya wanawake katika maandamano dhidi ya serikalai ya Sudan.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii