Wachina wafukuzwa Kenya kwa kuuza bidhaa sokoni kinyume cha sheria

Wakenya wanaouza bidhaa zao kwenye soko la Gikomba- Nairobi wanalalamika kuwa wafanyabiashara wa Kichina wanawaajiri wachina na kuleta ushindani wa b Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakenya wanaouza bidhaa zao kwenye soko la Gikomba- Nairobi wanalalamika kuwa wafanyabiashara wa Kichina wanawaajiri wachina na kuleta ushindani wa biashara

Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amewatimua nchini humo wafanyabiashara saba wa Kichina waliopatikana na hatia ya kufanya biashara zao kinyume cha sheria katika soko la maarufu kwa mitumba -Gikomba.

Hii ni baada ya Wakenya wanaouza bidhaa zao kwenye soko hilo lililopo jijini Nairobi kulalamikia ongezeko la Wafanyabiashara wa Kichina ambao walidai kuwa wanawaajiri wenzao na kuleta ushindani wa biashara.

Gikomba ni soko kubwa zaidi la nguo kuukuu au mitumba nchini Kenya.

Jumatano wiki hii Waziri wa mambo ya ndani alikuwa ameahidi kuwatimua wafanyabiashara wa kichina na wengine wa kigeni ambao watabainika kufanya biashara ndogo ndogo jijini Nairobi baada ya wakazi wa jiji hilo kulalamika kuwa Wachina wameleta ushindani mkubwa na wenyeji wanaofanya biashara katika masoko yanayouza nguo kuu kuu na bidhaa nyingine za bei za chini jijini humo ya Gikomba, Kamukunji na Nyamakima.

Haki miliki ya picha Wavuti wa wizara ya mambo ya ndani ya Kenya
Image caption Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amewaonya wafanyabiashara wa kigeni wanaoendesha shughuli zao bila vibali kuwa hawana nafasi nchini Kenya

"Raia wa kigeni kandaa wanaoshukiwa kufanya biashara nchini Kenya walikamatwa wakati wakati wa msako wa uvamizi wa katika soko la Gikomba. Wachina saba walibainika kukiuka sheria za uhamiaji.Maafisa walibaini kuwa watatu kati yao hawakuw ana vibali vya kazi huku wengine wakifanya kazi na shughuli nyingine zinazowaingizia mapato kinyume na vibali walivyopewa walipoingia nchini ,"ilisema taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani nchini kenya.

"kutokana na hayo, Waziri anayehusika na masuala ya uhamiaji ametia saini amri ya kuwarejesha makwao kulingana na sheria ."

Sheria ya uwekezaji nchini Kenya ya mwaka 2004 inawataka wawekezaji wa kigeni kufanya uwekezaji ambao ni lazima uwe wa manufaa kwa nchi katika kwa kuongeza kiwango cha taaluma miongoni mwa raia na kuboresha raslimali za nchi.

"Raia wa muombaji wa kibali cha uwekezaji nchini Kenya atapewa kibali hicho - iwapo atakuwa na walau dola elfu mia moja za kimarekani au pesa nyingine ya kigeni yeny ethamani hiyo ; awe na uwezo wa kubuni ajira kwa wakenya, kutoa ujuzi au teknolojia mpya kwa wakenya au ahamishie teknolojia kwa Wakenya na mambo mengine ambayo mamlaka zitaona kuwa ni ya maana kwa Kenya ," inaeleza sheria.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kwa kiasi kikubwa Wachina katika soko la Gikomba huuza nguo za mitumba, mazulia, na viatu kutoka Uchina

Wafanyabiashara katika soko maarufu la mitumba la Gikomba wanalalamika kuwa Wachina wanawaajiri Wachina wenzao kufanya kazi kama vile kupokea pesa na kuweka rekodi za mauzo, kazi ambazo hata Wakenya wanaweza kuzifanya, huku wakiwakodisha Wakenya kubeba mizigo kwa mikokoteni.

Kwa kiasi kikubwa Wachina katika soko la Gikomba huuza nguo za mitumba, mazulia, na viatu kutoka Uchina.

Katika masoko mengine ya Nyamakima na Kamukunji, Wachina huuza bidhaa za jumla kama vile nyaya za umeme, bidhaa za nyumbani, wanasesere na bidha nyingine ndogo ndogo za bei nafuu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii