Je ni kweli taasisi ya haki miliki ya muziki Kenya haiwalipi wasanii?

Wanamuziki wa kundi la Elani wanadai kushangazwa na malipo ya chini waliyopewa na Taasisi ya haki miliki ya muziki nchini Kenya Haki miliki ya picha Elanimuziki/Facebook
Image caption Wanamuziki wa kundi la Elani wanadai kushangazwa na malipo ya chini waliyopewa na Taasisi ya haki miliki ya muziki nchini Kenya

Taasisi ya haki miliki ya muziki nchini Kenya inakabiliwa na shutuma kali kutoka kwa wasanii wa muziki wanaodai limekuwa haliwalipi pesa zao kulingana na kazi yao.

Taasisi hiyo -Music Copyright Society of Kenya ina jukumu la kuwalipa wasanii wa muziki kwa kazi yao, lakini kwa miaka wasanii wa Kenya wamekuwa wakilalamika kuwa haliwalipi ili hali miziki yao inachezwa kwenye redio na televisheni.

Tulipe Pesa zetu, Tafadhali. Yamekuwa ni maneno yanayorudia mara kwa mara kila mara wanamuziki wanapokutana kwa mikutano yao na katika maandamano ya mitaani yanayolenga kupinga kutolipwa na taasisi hiyo. Hata hivyo bado hawajawahi kusikilizwa.

Na hata wale ambao wamewahi kulipwa wanadai walipewa pesa kidogo sana ambazo wanaziita''kichekesho'' ambazo hata ''hawawezi kuzitangaza kwa hadharani''

Wiki iliyopita kikundi cha wanamuziki cha Elani kilikuwa ndio cha hivi karibuni kabisa kuongeza sauti yao juu ya adha kuhusu malipo walitonayo wanamuziki kutokana na taasisi ya hati miliki ya muziki nchini Kenya , wakati walipofichua kuwa wamepokea shilingi 31,000 za Kenya tu kutoka kwa taasisi hiyo kwa miziki yao iliyochezwa kwenye vituo vya redio na televisheni kwa mwaka mzima .

Kwenye ukurasa wa Twitter, John K Mbindyo ametumia picha ya msanii wa Tanzania al maarufu Diamond Platnumz kuelezea mshangao wake juu ya malipo ya shilingi 31,000

Wajumbe watatu wa kikundi cha bendi ya Elani walishangazwa na kiasi hicho, ambacho kilionekana ni kidogo sana , ikilinganishwa na ubora wa nyimbo zao zilizopendwa kama vile Kookoo, Milele, Zuzu, Dunia ya Barua na Hapo Zamani ambazo zilitawala mawimbi ya vituo vya televisheni na redio .

Wanadai ya kuelezea malalamiko yao kuihusu taasisi ya MCSK, baadae walilipwa "fidia " ya Shilingi 300,000 za Kenya.

Kenye ukurasa wa Twitter, John K Mbindyo ametumia picha ya msanii wa Tanzania al maarufu Diamond Platnumz kuelezea mshangao wake juu ya malipo ya shilingi 31,000

Kutokana na video yao kwenye mtandao wa Youtube wakielezea masaibu yao, Wakenya alianzisha malalamiko yao kwenye mitandao ya haabari ya kijamii kupitia kampeni iliyoitwa #ElaniSpeaks ....Ikimaanisha #ElaniWaongea:

Kuongea kwa Elani, kuliibua gumzo, huku wasanii wengine wakichochewa kufichua kiwango kidogo cha pesa ambazo walilipwa awali kwa nyimbo ambazo zilikuwa maarufu nchini . Msanii Gidi Gidi alituma ujumbe wake wa Twitter uliosema: "nyinyi watu mna bahati mlilipwa Shilingi 31,000; nyakati zetu tulipata Shilingi 5,000 baada ya miaka miwili ya kibao Unbwogable,"

Haki miliki ya picha Pitson/Facebook
Image caption Mwanamuzi maarufu wa nyimbo za injili Lingala ya Yesu -Pitson alilipwa Shilingi 5,000 kwa wimbo huo ambao ulimpatioa umaarufu mkubwa

Msanii wa wimbo Lingala ya Yesu Pitson alilipwa Shilingi 5,000 kwa wimbo ambao ulimpatioa umaarufu mkubwa.

Boneye alipeleka masikitiko yake kwenye ukurasa wa Facebook alipokumbuka kwamba miaka mitatu iliyopita MCSK ilijaribu kulioa kikundi cha wasanii wa P-Unit Shilingi 250 kwa wimbo Kare, wimbo uliokuwa juu kwenye chati ya muziki wa Afrika wakati huo .Baada ya kukataa pesa hizo, pia walipokea shilingi 300,000 - kama tu Elani - na walitajwa kuwa ni kundi linalolipwa pesa ya juu zaidi la wasanii na taasisi ya MCSK.

Anasema anashukuru kwamba Elani ilizungumzia hili kwasababu watu wamekuwa wakijiuliza mbona wasanii wanalalamika ; lakini sasa umma umeona ni kwa nini hasa kuna malalamiko.

Haki miliki ya picha Sauti Sol /Facebook
Image caption Muimbaji wa Sauti Sol Bien anasema haoni jipya juu ya malalamiko yaliyotolewa dhidi ya MCSK

Licha ya kwamba hakufurahishwa na MCSK, muimbaji wa Sauti Sol Bien alishangazwa na jinsi watu walivyochagua kukasirishwa na utata usiomalizika wa taasisi hiyo. Na kwake alihisi Elani walitaka tu kusikika, jambo ambalo walilipata. Alidai kuwa MCSK imekuwa fisadi wakati wote.

Bien alifichua kuwa (Sauti Sol) hawasubiri huduma yake kwasababu shirika hilo silo litakalowatoa wasanii katika shida za pesa.

MCSK inasemaje juu ya shutuma za wasanii?

Likijibu malalamiko ya umma yaliyosababishwa na King Kaka, taasisi ya MCSK imeelezea kuwa sababu kuwa sababu wasanii wa kenya wanalipwa pesa kidogo ni kwasababu muziki wa Kenya hupewa muda muda mfupi sana wa kuchezwa kwenye vyombo vya habari.

Waliongeza kuwa ni nadra kwa watangazaji kulipia muziki walioucheza kwenye vituo vyao vya televisheni na radio, japo kwa muda mfupi wanaocheza.

MCSK imeelezea kuwa muziki wa Elani ulichezwa sana kwenye vyombo mba vya habari, lakini vile alivyovitaja kuwa "watangazaji wakuu ". Hata hivyo, muziki yao hjaikuchezwa kweney vituo vya redio vya lugha zinazozungumzwa nchini.

Kuhusu fidia ya Shilingi 300,000 iliyotolewa kwa Elani , MCSK inasema kwamba wamekuwa wakitoa malipo kwa wajumbe ambao wametoa na kuthibitisha kwamba kulikuwa na kuchelewa kwa upakuaji wa muziki au kushindwa kupakuliwa kw amuziki katika mfumo wa ufuatiliaji wa mafanikio ya muziki

"Si ukweli kwamba Elani ''waliitwa tu'' baada ya wiki moja na kulipwa shilingi 300,000 bali kulikuwa na mchakato uliofuatwa, uliopeleka Elani kulipwa ," ilieleza MCSK.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Nchini Burundi wanamuziki maarufu wa kike ni wachache kwa sababu ya vikwazo vya tamaduni

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii