Tetesi za soka Ulaya Jumapili 08.09.2019: De Gea, Mbappe, Neymar, Skriniar, Van der Sar

kipa wa Manchester United, David de Gea
Image caption Kipa wa Manchester United, David de Gea

Timu inayoshiriki ligi ya nchini Italia ,Juventus ipo mbioni kufungua mazungumzo na kipa wa Manchester United, David de Gea Januari 2020, tayari Klabu ya Manchester United imeanza kutafuta mrithi wa muhispania huyo.(Sunday Express)

United iko mbioni kukamilisha dili la kumteua kipa wa Zamani wa timu hiyo Edwin van der Sar kuwa Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Vaadhi ya wachezaji wa Barcelona walijitolea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Brazil Neymar Jr. (Marca)

Mawakala wa soka wameambiwa wajiandae kufanya dili za maana mwezi Januari ndani ya Chelsea. (Sunday Mirror)

Klabu ya Manchester City imejiandaa kutuma dau la pauni milioni 24 kwa mlinzi wa Slovakia na Milan kwa ajili ya kumaliza tatizo la majeruhi ndani ya klabu hiyo. (Sunday Express)

Virgil van Dijk, 28, mchezaji bora wa Uefa amekubali kuongeza mkataba wa miaka sita kuitumikia klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Real Madrid bado inahaha kupata saini ya kinda wa Kifaransa Kylian Mbappe, 20, kutokea Paris St-Germain dirisha la usajili msimu ujao. (Sport - in Spanish)

Strika wa Mexico Javier Hernandez, 30, angesalia West Ham kama angekubali kuongeza mkataba wa kubakia kwa wagonga nyundo hao wa London. (Football London)

Kiungo wa Tottenham raia wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 22, ameanza kujifunza lugha ya kiingereza ili kujichanganya vyema na wachezaji wenzake London baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Lyon. (Football. London)

Strika wa Roma Edin Dzeko amesema amefarijika kujumuika pamoja na mchezaji mpya ndani ya klabu hiyo Henrikh Mkhitaryan, 30-ayejiunga na timu hiyo kutokea Arsenal. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Winga wa Juventus Juan Cuadrado, 31, amesitisha mazungumzo na klabu hiyo kutokana na kutopata muda wa kutosha klabuni hapo chini ya Maurizio Sarri. (Goal)

Kinda wa England Eddie Nketiah, 20, ameenda kwa mkopo Leeds United kutokea Arsenal kwa ajili ya kupata nafasi kubwa ya kuonyesha uwezo wake. (Mail on Sunday)

Meneja wa Sevilla Julen Lopetegui alihitaji kumsaini mlinzi wa Hispania Nacho Fernandez, 29, kutoka kwa wapinzani wao Real Madrid kwenye dirisha kubwa la usajili. (Marca)

Mshambuliaji wa timu ya taifa Mexico Javier Hernandez (30) angebakia kwente klabu ya West Ham mpaka mwisho wa mkataba wake kama Sevilla wasinge tangaza dau lakumnunua katika wiki ya mwisho ya usajiri.(Football Italia)

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa Ufaransa na meneja wa timu ya wanawake Lyon Raynald Pedros yupo kwenye mazungumzo na chama cha Soka cha Korea Kusini.(L'Equipe - in French)

TETESI ZA JUMAMOSI

Lionel Messi ataruhusiwa kuondoka Barcelona bila malipo yoyote msimu ujao , iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atapendelea kufanya hivyo kutokana na kifungu cha sheria katika kandarasi yake. (El Pais, via L'Equipe)

Messi ataruhusiwa kuzungumzia hatma yake na klabu yoyote kutoka Januari mosi. (Marca - in Spanish)

Mabingwa hao wa Ufaransa waliwaonya Barcelona kuhusu lengo hilo la Real Madrid wakati wa mazungumzo ya vilabu hivyo viwili kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu huu.. (Sport - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji wa Brazil Neymar atalazimika kusalia PSG hadi pale atakapokubali kupunguza marupurupu yake kulingana na rais wa La Liga Javier Tebas. (Mail)

Chris Smalling yuko tayari kuondoka Man United baada ya beki huyo mwenye umri wa miaka 28 kujiunga na klabu ya Roma kwa mkopo. (Mirror)

Na Beki wa United raia wa Argentina Marcos Rojo, 29, yuko tayari kupigania uhamisho wa mwezi Januari mbali na klabu hiyo iwapo atahitajika kufanya hivyo baada ya uhamisho wake wa kuelekea Everton kugonga mwamba. (Ole - in Spanish)

Mabingwa wa Itali Juventus wanafikiria kumnunua beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27.

Real Madrid itamwania mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe msimu ujao .

Inter Milan pia wana hamu ya kumsajili Alderweireld. (Mail)

Mabingwa wa Uhispania Barcelona walitaka kumsaini winga wa Itali mwenye umri wa miaka 25 Federico Bernardeschi kutoka Juventus katika dirisha la uhamisho la msimu huu (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii