Italia: Mabaki ya kale ya waliodhaniwa wapenzi yabainika kuwa ya jinsia moja

Skeleton Haki miliki ya picha Archeomodena
Image caption Mabaki ya wapenzi wa jinsia moja waliokufa wakiwa wameshikana mikono yapata miaka 1500 iliyopita

Watafiti wamebaini kuwa mabaki ya miili ya watu wa kale waliokuwa wameshikana mikono yaliyopatikana Roma , Italia , wote walikuwa wanaume.

Masalio ya mabaki hayo yalijulina kama 'Lovers of Modena'.

Watafiti hawakuweza kugundua jinsia za mabaki hayo wakati walipoyagundua nchini Italia mwaka 2009 kwa sababu walikuwa hawajahifadhiwa vizuri.

Lakini njia mpya ya utafiti wa utafiti wa protini katika meno, umeweza kubainisha jinsia zao.

Uhusiano wa mabaki haya ya watu wa kale ya karne ya 4 mpaka 6 bado haujafahamika.

Watafiti wanasema kuwa wanaume hawa walizikwa wakiwa wameshika mikono.

Haki miliki ya picha Archeomodena
Haki miliki ya picha Archeomodena

Baadhi ya watafiti walihusisha mabaki hayo kwa kudai kuwa walikuwa ndugu au wanajeshi waliokufa pamoja katika vita.

Watafiti hawa wanahusisha vita kwa sababu makaburi mabaki hayo yalipatikana katika makaburi ya vita.

Haki miliki ya picha Archeomodena

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii