Ushaidi wa kwanza wa matumizi ya maziwa watolewa

Neolithic jaw Haki miliki ya picha Sophy Charlton / Dorset County Museum
Image caption Ushaidi huo unaonekana kwenye meno ya masalio ya watu wa kale

Wanasayansi wamegundua ushaidi wa kale zaidi wa lini maziwa ya wanyama wa kufugwa yalianza kutumika na binadamu.

Watafiti hao walibaini kutoka kwenye masalio ya meno ya mtu wa kale wa zamani kutoka nchini Uingereza.

Utafiti unaonyesha kuwa bidhaa za maziwa na maziwa yenyewe yalianza kutumiwa na binadamu miaka 6000 iliyopita.

Waliweza kutumia maziwa kutengeneza jibini(cheese), maziwa ya mgando na bidhaa nyingine.

Na kadri siku zilivyosogea walipunguza kiasi cha maziwa ambayo walitumia.

Watafiti hao walisugua masalio ya meno ya watu kadhaa na walitenganisha sehemu tofauti ndani yake na kuzichambua kwa ustadi mkubwa.

Waliweza kuona protini ya maziwa inayoitwa 'beta-lactoglobulin (BLG)' kutoka kwa watu saba wa kale.

Dkt Sophy Charlton kutoka idara ya mambo ya kale, anasema ugunduzi huu ni suala la kihistoria ambalo limefanyiwa utafiti hivi karibuni.

Haki miliki ya picha University of York
Image caption Dkt Charlton akionyesha sampuli waliyopata inaonyesha kuwa tayari walianza kutengeza chakula kwa maziwa

Na ugunduzi huu ulianza kwa kuchunguza namna ambavyo watu wa kale walivyoweza kutumia sukari iliyomo kwenye maziwa tofauti na wao kunywa wakiwa watoto.

Ingawa matumizi ya maziwa katika chakula yalikuwa yanawafanya wapate maumivu ya tumbo , kuhara na kupata kichefuchefu.

Ingawa bado watu wengi wa siku hizi wanatengeneza vyakula kwa maziwa na kutumia hata wakiwa na rika la utu uzima .

Mabadiliko hayo yameathiri sehemu ya vina saba kuweza kukabiliana na uzio ambao unaweza kumpata mtu kutokana na matumizi ya maziwa.

Licha ya kwamba utafiti wa nyuma haukuonyesha mabadiliko hayo .

Dkt. Charlton anasema inawezekana watu wa zamani walikuwa wanajizuia wenyewe kunywa maziwa kwa kiwango kikubwa.

"Kama ni kweli walikuwa wanatumia kiwango kidogo sana cha maziwa, yasingeweza kuwafanya watu kuumwa," alieleza.

Lakini pia aliongeza kuwa kama walikuwa wanatengeza jibini, maziwa ya mgando basi hata kiwango cha maziwa kilikuwa kinapungua.

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Binadamu wa kale walianzisha ufugaji wa kondoo, ng'ombe na mbuzi.

Utafiti umeonyesha ushaidi wa mifugo ya wanyama ambao walikuwa wanatoa maziwa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa za maziwa.

Wanadamu wa kale huko nchini Uingereza kutoka miaka ya 6000 mpaka 4000 iliyopita walianzisha kilimo wakiwa wanafuga wanyama wafugwao nyumbani kama ng'ombe, kondoo, nguruwe na mbuzi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii