Matangazo ya uongo ya video za matibabu ya saratani kunufaisha mtandao wa Youtube

bbb Haki miliki ya picha YouTube’s algorithm promotes medical misinformatio

Uchunguzi uliofanywa na BBC, umebaini kuwa kuna video za lugha mbalimbali katika chaneli za Youtube, zinazotoa taarifa ambazo sio sahihi za matibabu ya saratani.

Na matangazo mengine yanayoongoza kwa taarifa za uongo ni video za bidhaa mbalimbali na vyuo vikuu.

Katika lugha 10 zilizopo Youtube, BBC ilibaini zaidi ya video 80 ambazo zina maudhui ya afya ambayo sio sahihi haswa ya ugongwa wa saratani.

Katika video 10 zilizochunguzwa tayari watu zaidi ya milioni wameangalia.

Wengi walivutiwa na matangazo hayo.

Tiba ambazo hazijathibitishwa ambazo zinadai kuwa vitu kama ukwaju au amira kuwa tiba.

Juisi au kufunga ni miongoni mwa tiba zilizokuwa zinafundishwa katika video hizo.

Watumiaji wengine wanahamasisha watu kunywa maziwa ya Punda huku wengine wakitaka watu wanywe maji ya moto.

Huku hakuna hata tiba yeyote kati walizotaja imethibitishwa kitaaluma kuwa inatibu saratani.

Inaonekana kuwa kuna video nyingi zinazotangaza tiba ya uongo ya saratani pamoja na matangazo ya bidhaa kama Samsung na Heinz.

Matangazo yaliyopo Youtube huwa yanainufaisha kampuni ya Google pamoja na waliotengeneza video za uongo.

Haki miliki ya picha YouTube
Image caption Khawla Aissane, akiongea kwa lugha ya kiarabu akiongea katika chaneli yake ya Youtube kuwa maziwa ya Punda yanaweza kuponya kansa.

Mwezi Januari , Youtube ilitangaza kuwa itaziondoa video ambazo zina maudhui ambayo si rafiki kwa mtazamaji kwa moja ama nyingine haswa video zinazodai kutoa tiba za miujiza kwa magonjwa hatari.

Kampuni hiyo ilijaribu kutatua tatizo kwa video za kiingereza tu na haikutilia maanani lugha nyingine.

BBC ilifanya uchunguzi katika lugha ya Kiingereza, Kireno, Kiarabu, kirusi, kihindi, Kifaransa, Kijerumani na Kiitaliano.

Kwa mfano katika lugha ya Urusi, watu wanahamasishwa kunywa maji ya amira kama tiba ya kansa.

Video hiyo ilikuwa inawashauri watu kufunga kula na kunywa juisi ya karoti .

Pamoja na kwamba Youtube imekataza maudhui ambayo yanaweza kuleta madhara kwa binadamu kwa kuhamasisha maudhui ya uongo lakini bado changamoto ni kubwa.

Kwa sababu inaonekana kuwa kuna wengi wanaoamini tiba hizo za uongo na hata kutozingatia tiba sahihi.

Haki miliki ya picha YouTube
Image caption watumiaji wengi wa Youtube Brazi wanahamasisha watu tiba za asili za uongo za saratani

Fedha nyingi zinapatikana katika video zenye maudhui ya uongo

Watafiti kutoka BBC Monitoring na BBC news Brasil walikuwa walipata athari mara baada ya video za uongo za tiba kuanza kusambaa.

Pamoja na matangazo ya kliniki, Samsung na Heinz , BBC iliona pia matangazo ya programu za kushihisha maneno, kukata tiketi katika mitandao, filamu za Hollywood pamoja na vyuo vikuu.

Video zote zilikuwa na taarifa zisizo sahihi.

Kampuni na Vyuo, vimejiweka mbali katika maudhui hayo ya uongo na kudai kuwa hawana uhusiano wowote.

Haki miliki ya picha YouTube
Image caption Efimova Tatyana, video yake iliondolewa kwa sababu ilikuwa inahamasisha kuwa amira ni dawa ya saratani

Wataalamu wa afya wanasema kuwa ili kupata seheme ya suluhisho ni vyema watengenezaji wa maudhui ya afya wafanye kazi na wataalamu wa tiba.

"Kuna umuhimu wa elimu kutolewa ili wataalamu wa afya kufanya kazi na watayarishaji vipindi, ingawa sina uhakika kama kuna uwekezaji wa kutosha", Mtaalamu wa afya alisema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii