Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 03.10.2019:Maddison, Pochettino, Badiashile, Kante, Rice, Upamecano

Mchezaji N'Golo Kantemwenye umri wa miaka 28. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo mkabaji N'Golo Kante,28, kuelekea Juventus?

Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri ana matumaini ya kuungana tena na kiungo mkabaji N'Golo Kante, 28. Sarri ambaye kwa sasa anainoa Juventus yupo tayari kumnunua kiungo huyo raia wa Ufaransa kwa kitita cha takribani pauni milioni 70. (Mail)

Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kama sehemu ya kufufua kikosi cha Manchester United. (Manchester Evening News)

Manchester United pia wanaendelea kumfuatilia kiungo wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison, 22, ambapo wanaweza kumsajili kwa pauni milioni 80. (Mail)

Haki miliki ya picha Juan Manuel Serrano Arce/Getty Images
Image caption Ousmane Dembele

Mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 24, anaamini wakati wa klabu yake kushinda michuano ya Champions League umekaribia, japo amewaasa wachezaji wenzake kusalia na subira.. (Mirror)

Wachezaji wa Tottenham wanahofu juu ya mustakabali wa wa kocha wao Mauricio Pochettino, na wanaamini raia huyo wa Argentina anatafuta njia ya kuondoka klabuni hapo. (Mail)

Mshambuliaji fundi wa zamani wa Spurs na Manchester United Dimitar Berbatov anaamini mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy atafanya mazungumzo na Pochettino "wiki hii" ili "kupata majibu sahihi na njia muafaka ya kusonga mbele." (Star)

Image caption Je Ole Gunnar Solskjaer ataweza kibadili Manchester United

Kocha wa Arsenal Unai Emery amesema mshambuliaji wake raia wa Ivory Coast Nicolas Pepe anatakiwa kujifunza kustahamili presha ya kuwa mchezaji wa Arsenal. Pepe, 24, amesajiliwa na Arsenal kwa rekodi ya kitita kinono zaidi cha pauni milioni 72 mwezi Agosti akitokea klabu ya Lille. (Mirror)

Beki wa Tottenham Toby Alderweireld, 30, amekiri kuwa klabu hiyo imeporomoka kiwango zaidi sasa kuliko kipindi chochote katika miaka mitano iliyopita. Kikosi hicho kipo nyuma ya vinara wa ligi Liverpool kwa alama 10, wametolewa kwenye kombe la Corabao na klabu ya dara ja la pili Colchester na wakaadhibiwa vikali kwa goli 7-2 na Bayern Munich kwenye Champions League juzi Jumanne. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino

Baada ya kipigo kutoka Bayern, kocha wa Tottenham Pochettino alifanya mazungumzo ya dharura kwenye vyumba vya kubadili nguo, na aliendeleza mazungumzo hayo wakatii wa mazoezi jana Jumatano. (Mirror)

Chelsea wanampango wa kumsajili beki wa kati kinda kutoka klabu ya Monaco Benoit Badiashile, 18, mwezi Januari endapo watafanikiwa kuruhusiwa kufanya usajili. (Le 10 Sport, via The Sun)

West Ham wamemkadiria thamani ya pauni milioni 80 kiungo wao Declan Rice, 20, kufuatia tetesi kuwa anatakiwa na klabu ya Manchester United. (Star)

Bayern Munich wanataka kumsajili mchezaji kinda na nyota wa Birmingham Jude Bellingham, 16, na kumfanya nyota wao wa baadae kutoka England. (Sun)

Arsenal wanaweza kumsajili beki wa RB Leipzig Dayot Upamecano, 20, mwezi Januari kwa kitita cha pauni milioni 53 baada ya kushindwa kumnunua kwenye dirisha la usajili lililopita kwa kuishiwa bajeti. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii