Upinzani Uganda wagadhabishwa na uvamizi wa wanajeshi katika Chuo kikuu

Polisi wakishika doria karibu na Chuo Kikuu cha Makerere
Maelezo ya picha,

Mapema wiki hii makumi kadhaa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere walikamatwa na polisi walipokuwa wakiandamana kuomba kupunguzwa kwa karo ya shule

Wanafunzi nchini Uganda wameripotiwa kujeruhiwa baada ya jeshi la nchi hiyo kufanya uvamizi wa usiku katika mabweni yao katika Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo katika ya mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.

Wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wameelezea hasira zao baada ya kugundua kuwa wanafunzi wamelazwa hospitalini kwa madai ya kupigwa na wanajeshi.

Unaweza pia kusikiliza:

Polisi waliingilia kati na kuuvunja mkutano wa wandishi wa habari katika chuo hicho ambapo viongozi wa wanafunzi walikuwa wakitoa maelezo kuhusu uvamizi huo.

Video hii iliyotumwa kwenye ukurasa wa Twitter na televisheni ya kibinafsi ya NTV imesema kuwa jeshi la Uganda linawashikilia wanafunzi 46 wa Chuo Kikuu cha Makerere kufuatia maandamano ya wanafunzi juu ya karo na wengine takriban 11 wamelazwa baada ya jeshi na polisi kuvamia mabweni ya kulala ya wanafunzi:

Televisheni hiyo pia inaonyesha polisi wakichukua vinasasauti (microphones) na kumtaka kila mmoja aondoke.

Mwalimu katika chuo hicho kitiovo cha sheria Profesa Ben Twinomugisha kupitia ukurasa wa Facebook amelaani uvamizi huo na akasema hawezi kwenda katika Chuo hicho akijifanya kuwa mambo ni ya kawaida. Amesema kuwa kinachoendelea katika bweni la Lumumba chuoni hapo kinamkumbusha ukatili wa wanajeshi wa Amin walioutekeleza kwa wanafunzi na wahadhili.

Mapema wiki hii makumi kadhaa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere walikamatwa walipokuwa wakiandamana kuomba kupunguzwa kwa karo ya shule.

Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda walivamia kituo cha polisi, wakidai kuachiliwa huru kwa wenzao 15 waliokamatwa walipokuwa wakiandamana dhidi ya kuongezeka kwa karo ya masomo iliyoidhinishwa mwaka jana.

Maelezo ya picha,

Uvamizi wa wanajeshi wa Uganda katika mabweni ya Chuo Kikuu cha Makerere ulifanyika usiku

Wanafunzi 15 walikamatwa siku ya Jumatatu walipokuwa wakijaribu kuandamana kuelekea katika ofisi ya rais Yoweri Museveni kumuomba aingilie kati mzozo huo.

Picha zilizotumwa kwenye mtandao wa Twitter zilionyesha wanafunzi hao wakikamatwa nje ya lango la Chuo kikuu na wanajeshi pamoja na polisi.

Unaweza pia kusikiliza:

Maelezo ya sauti,

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere, anatarajiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Picha zilizotumwa kwenye mtandao wa Twitter zilionyesha wanafunzi hao wakikamatwa nje ya lango la Chuo kikuu na wanajeshi pamoja na polisi.