Gumzo mtandaoni lahoji miundo mbinu gani ilipaswa kupewa kipaumbele Tanzania

Ndege

Chanzo cha picha, Ikulu, Tanzania

Wakati mvua zikiwa zinaendela kunyesha maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kusabisha vifo, uharibifu wa miundombinu na kero kwa wananchi katika makazi yao.

Mwishoni mwa wiki mvua hizo zimesababisha kukatika kwa barabara kubwa kadhaa na kusabisha watu kulala njiani kwa zaidi ya siku mbili.

Kufikia siku ya jumatatu, watu waliofariki kuanzia ijumaa wamefikia 15 mpaka hapo jana katika maeneo ya Tanga, kamanda mkuu wa polisi mjini Tanga amethibiti hilo.

Licha ya kwamba maafa ya mafuriko katika taifa hilo sio jambo geni lakini mjadala umeibuka kwa baadhi ya watu kulalamikia juu ya ndege zinazonunuliwa huku barabara bado ni changamoto.

Baadhi ya watu wameonekana wakibeza ujio wa ndege mpya wakati ambao watu wanahangaika katika usafiri wa barabara.

Huku wengine wakiwa hawaoni umuhimu wa manunuzi ya ndege nyingi huku wananchi wengi wakiwa bado wanatumia usafiri wa barabara.

Chanzo cha picha, IKULU,TANZANIA

Wengine wakihoji kama rais akiacha kuagiza ndege , je mafuriko hayatakuepo?

Madai hayo yakitajwa kuwa mbinu za wapinzani huku wakihojiwa kama nchi nyingine gani mafuriko hayapo?

Tanzania imepokea ndege nyingine kubwa aina ya Boeing 787 Dreamliner kutoka nchini Marekani siku ya jumamosi.

Ndege hiyo ilipokewa na rais John Pombe Magufuli aliyewaongoza mamia ya watanzania katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere .

Ndege hiyo ni ya saba kati ya 11 zinazotarajiwa kununuliwa na serikali kufikia mwaka 2022.

Ndege ambazo zimewasili nchini Tanzania kufikia sasa:

1. Ndege 2 aina ya Boeing 787-8

2. Ndege moja aina ya Forker 50

3. Ndege 3 aina ya Bombardier Dash 8-400

4. Ndege nyingine moja aina ya Bombardier Dash 8-300

5. Ndege 2 aina za Airbus A220-300