Watoto wanaweza kuhesabu kabla ya kufundishwa

Infant who took part in the counting experiment

Chanzo cha picha, Johns Hopkins University

Maelezo ya picha,

Utafiti umebaini kuwa watoto wadogo wana uwezo wa kuhesabu hata kabla ya kufundishwa

Watoto wadogo wenye umri kuanzia miezi 14 wana uwezo wa kuhesabu hata kabla hawajaanza kuelewa umuhimu wa kujifunza kuhesabu moja, mbili, tatu ; wanasayansi wanasema.

Watafiti hao kutoka Marekani wanasema kuwa watoto wanaweza kusikia hesabu zinazotamkwa kwa sauti kubwa na kutambua idadi yake.

Ikiwa watoto wengi huwa hawaelewi namba hizo huwa zina maana gani mpaka wanapofikia umri wa miaka minne.

Wanasayansi sasa wanataka kuona kama uwezo wa watoto kuhesabu wakiwa wadogo huwapelekea na utaalamu wa kuhesabu siku za mbeleni.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha John Hopkins, watoto kumi na sita ambao walikuwa wanawaangalia wanasesere wanne-huku mbwa mdogo na gari-walikuwa wamefichwa kwenye sanduku.

Muda ambao watafiti wlihesabu kwa sauti, wanapodondosha mwanasesere mmoja na husema, angalia - moja, mbili, tatu, nne. Mbwa wanne."

Wakati mwingine, watafiti huwa wanasema : Hii, hii ,hii- au hawa mbwa."

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wanasesere wamehesabiwa , watoto huwa wanatarajia kuwa ni zaidi ya mwanasesere mmoja ndio anaweza kutolewa kwenye sanduku.

"Watoto hawa hawakuweza kuhesabu namba sahihi lakini walikuwa wanakumbuka namba sahihi ambazo wamehesabu", watafiti walisema.

Lakini wakati wanasesere hao wakiwa hawahesabiwi, watoto wanahisi kuvurugwa pale watafiti wanapodondosha mdoli mmoja , na kuangalia kama hawaoni kitu kingine chochote.

Mtafiti Jenny Wang anasema kuwa wakati wanapowahesabu wanasesere kabla hawajawaficha, huwa wanaonekana kukumbuka wanasesere wangapi walikuepo kabla."

Mtafiti anasema kuwa alishangazwa sana kuona namna watoto wachanga wanavyoweza kuhesabu huku watu wengine, kuhesabu huwa sio jambo rahisi".

Watafiti wanaamini kuwa watoto wadogo wanaweza kuanza kufundishwa kuhesabu wakiwa wadogo zaidi hata kabla ya umri wa kuanza shule za awali.

Timu ya watafiti wanataka kujua kama watoto hao wanao-ongea kiingereza wanaweza kuhesabu kwa lugha za kigeni.

Utafiti huu umechapishwa katika jarida la maendeleo ya sayansi.