Kwamboka Kibagendi aliyezaliwa na jinsia mbili aelezea masaibu yake

Changamoto aliyokumbana nayo Kwamboka Kibagendi ilikuwa ni kushindwa kwake binafsi kujua utambulisho wake kinjisia

Chanzo cha picha, Kwamboka Kibagendi

Maelezo ya picha,

Changamoto aliyokumbana nayo Kwamboka Kibagendi ilikuwa ni kushindwa kwake binafsi kujua utambulisho wake kinjisia

Kwamboka Kibagendi ana umri wa miaka 30, alizaliwa na jinsia mbili ya kike na ya kiume ama Huntha kutoka Nairobi Kenya , maisha yake yamekuwa ya hisia mchanganyiko.

Changamoto hii ilitokana na kushindwa kwake binafsi kujua utambulisho wake kijisia.

Alishindwa kubaini ikiwa yeye ni mume au mke jambo lililomfanya kuwa na mawazo mengi wakati alipokuwa akikua.

Kwamboka ni jina la kike kutoka Kusini Magharibi mwa Kenya eneo la Kisii , na huko ndipo alipozaliwa.

Wazazi wake walifariki akiwa mdogo kwa hiyo hakuwa na nafasi ya kujielewa vyema kwani wazazi wake hawakuwa hai kumsaidia kujielewa.

Alilelewa na bibi yake na hakuhisi kuwa na uhuru wa kuzungumza nae wazi kuhusu hali yake ya kijinsia na ili kuelewa ikiwa yeye ni msichana au mvulana.

Chanzo cha picha, Kwamboka Kibagendi

Maelezo ya picha,

Kwamboka Kibagendi hakuhisi kumuelezea mtu yeyote juu ya masaibu ya utambulisho wa jinsia yake

Anasema kuwa kile ambacho kimefichwa na nguo wakati mwingi kinakuwa ni siri ya mtu binafsi kwa hio hakuna mtu aliyemuelewa naye pia hakujielewa.

Alipoingia shule ya Sekondari alikuwa anapenda kucheza soka , na alipowekwa kwenye timu za wasichana, ambapo alilicheza soka kwa umahiri kama mvulana kutokana na nguvu na mtindo wake , na hilo lilimfanya abandikwe majina mengi shuleni.

''Hali hii ya kuwa na jinsia mbili sio rahisi...tayari wazazi wangu walikuwa wamenichagulia utambulisho wangu... Walinitambua kama mvulana'', anasema Kwamboka.

Kupitia mtandao ameweza kusoma na kuelewa zaidi kuhusu hali yake ya kuwa huntha.

Unaweza pia kusoma:

Masaibu kuhusu utambulisho wa jinsia aliyokumbana nayo Kwamboka Kibagendi , hayatofautiani sana na yale aliyoyapata Mkenya mwenzake Mary Waithera ama James Karanja.

Kulikuwa na hali ya switofahamu wakati Mary Waithera ama James Karanja alipozaliwa mwaka 1991, wakunga walinyamaza wasijue cha kumwambia mama yake.

Alizaliwa na jinsia mbili...jinsia ya kiume na ya kike kwa pamoja.

Mama yake akitaka kupata kujua mbona mwanae akazaliwa katika hali hiyo?. Shughuli zote za kutanzua hali hii zilimfanya Mary kulazwa hospitalini kwa wiki tatu alipozaliwa.

Huo ukawa ndio mwanzo wa safari ya Mary Waithera ama James Karanja kujitambua

Wazazi wa Mary Waithera waliamua kuanza kumlea kama msichana.

Maelezo ya picha,

Mary Waithera ama James Karanja kutoka Kenya pia alizaliwa na jinsia mbili

Mary Waithera ama James Karanja anasema kulikuwa na hali ya sintofahamu wakati Mary Waithera ama James Karanja alipozaliwa mwaka 1991, wakunga walinyamaza wasijue cha kumwambia mama yake.

Alizaliwa na jinsia mbili...jinsia ya kiume na ya kike kwa pamoja. Mama yake akitaka kupata kujua mbona mwanae akazaliwa katika hali hiyo?. Shughuli zote za kutanzua hali hii zilimfanya Mary kulazwa hospitalini kwa wiki tatu alipozaliwa. Huo ukawa ndio mwanzo wa safari ya Mary Waithera ama James Karanja kujitambua

Wazazi wa Mary Waithera waliamua kuanza kumlea kama msichana.

Nilizaliwa tatizo

''Kutoka Mwanzo ,nilizaliwa kuwa tatizo,angalaua kulingana na wale waliokuwa karibu nami. Hakuna aliyejua nilikuwa nini'', anasema James Karanja.

Baada ya wazazi wangu kutambua kuwa nilikuwa na matatizo hayo,Babangu aliamua,waliamua kunilea akama msichana ili iwapo siku za usoni nitabadilika na kuwa manaumme,basi itakuwa rahisi kufanya hivo.

Hata hivyo hali yangu ilifanya ndoa ya wazazi kuvunjika.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Kizungumkuti cha kujaliwa watoto wenye jinsia mbili