Mwanaume mjini Moscow anakabiliwa na kifungo kwa kumtishia polisi paka

An angry cat (stock photo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Paka alidaiwa The cat was said to have scratched the police officer's face after being thrown (stock photo)

Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa mwanaume mmoja mjini Moscow anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kumtumia paka kama silaha yake.

Mtuhumiwa huyo Gennady Shcherbakov anatuhumiwa kwa kumrushia polisi paka wakati ambapo polisi alikuwa ameenda kuthibiti keleleambazo zilikuwa katika makazi ya watu.

Bwana Shcherbakov, 59, anakabiliwa na kosa la jinai la unyanyasaji dhidi ya polisi.

Kesi hiyo ilifunguliwa siku ya jumatano, ambapo ilikuwa ni kipindi cha zaidi ya mwaka tangu tukio hilo litokee , imeripotiwa na chaneli ya Telegram Baza

Tuhuma hizo zilikuwaje?

Kwa mujibu wa teevisheni ya taifa ya Urusi, tarehe 4 oktoba 2018, bwana Shcherbakov alikuwa amekuwa anapiga kelele katika makazi ya watu huko Moscow.

Anadaiwa kuwa alikuwa amelewa sana.

Wakazi wa eneo hilo waliripoti kuhusu usumbufu aliokuwa anasababisha ,

Mara baada ya polisi kufika katika eneo hilo kumzuia asiendelee kufanya fujo , bwana Shcherbakov aligoma kutoa ushirikiano kwa polisi na hata kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa.

Badala yake bwana Shcherbakov anadaiwa kuwa a limnyanyua paka ambaye alikuwa karibu yake na umrushia polisi.

Mnyama huyo anaripotiwa kuwa alimjeruhi polisi.

Bwana Shcherbakov, ambaye hakuwa mkazi wa eneo hilo, anakanusha kuhusika na tukio hilo na hata kutumia paka kama silaha.

Yeye anadai kuwa paka huyo alimrukia polisi mwenyewe bila kurushwa au kusukumwa na mtu yeyote.

Kesi hiyo imewekwa kwenye kifungu cha 318 , kwa kosa la uhalifu wa jinai wa kutumia vurugu dhidi ya asifa wa umma.

Haijafahamika kwa nini kesi hiyo imechukua muda mrefu kufunguliwa kama kosa la jinai na hata hawajaeleza nini kitamkuta paka aliyehusika