Je sanaa ya Cuba inawasilisha vipi mapambano ya ukombozi wa Afrika?

Haki miliki ya picha Lázaro Abreu Padrón

Maonyesho ya vipeperushi vya matangazo ya propaganda za Cuba huko London yanaonyesha msaada ambao Fidel Castro alitoa kwa harakati za ukombozi wa Afrika wakati wa vita baridi.

Kazi za sanaa zilizotengenezwa katika kampuni ya Castro ya mshikamano wa watu wa Asia, Afrika na Amerika ya Kusini (Ospaaal) ambayo ilianzishwa mwaka 1966 huko Havanna katika mkutano wa 'Tricontinental' kwa lengo la kupambana na ukoloni wa Marekani.

"Nchi nyingi za Afrika ziliwakilishwa kama wajumbe katika harakati za ukombozi. Vilevile Castro alisaidia kuwaunganisha baadhi ya viongozi haswa kutoka Guinea-Bissau," Olivia Ahmad, miongoni mwa wachoraji aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha Olivio Martínez Viera
Image caption Amílcar Cabral akiwa anahamasisha mshikamano wa watu wa Guinea-Bissau na kisiwa cha Cape Verde, 1974

Cabral aliongoza mapigano dhidi ya ukoloni wa Ureno huko Guinea-Bissau na kisiwa cha Cape Verde, lakini aliuwawa mwaka 1973, mwaka mmoja kabla Guinea-Bissau kupata uhuru.

Bi Ahmad anasema kuwa mkutano ule wa Tricontinental ulikuwa umepangwa kufanyika lakini haukufanyika hivyo ukachapishwa.

Hivyo machapisho yake kuwa kiungo muhimu cha taarifa na uwasilishi.

Mapinduzi ya Amerika Kusini yalijulikana zaidi, Ernesto "Che" Guevara, labda alikuwa mpambanaji zaidi katika harakati hizo.

"Lakini pia kuna viongozi wa kiafrika ambao wamekuwa wakikumbukwa kwa ushujaa wao "

Haki miliki ya picha Alfredo G Rostgaard
Image caption Che Guevara imeonyeshwa kwenye bango la mwaka 1969

Guevara aliipambania nchi ambayo inatambulika sasa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo mwaka 1965 ,kwa dhamira iliyoshindwa ya kuchochea uasi dhidi ya utawala wa kigeni wa miaka minne baada ya kuuawa kwa shujaa wa uhuru wa Kongo, Patrice Lumumba.

Lumumba aliuwawa miezi minne baada ya kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza kidemokrasia katika taifa lake, jambo ambalo lililaumiwa na wanaintelijensia wa Marekani na Uingereza.

Haki miliki ya picha Alfredo Rostgaard
Image caption Patrice Lumumba , 1972

"Michoro hiyo inavutia kwa sababu kwa sababu ya sanaa yake ya ushawishi ambao huwezi kutarajia kuuona, michoro hii ina muonekano wa kuwaenzi kwa furaha watu ambao walijitoa mhanga ili kuleta ukombozi," anasema bi Ahmad.

Maonyesho haya ya picha yaliobuniwa Cuba, yaliandaliwa na wabunifu 33 na wengi wao wakiwa wanawake.

Picha kuhusu Guinea-Bissau inamuonyesha mwanamke akiwa ameshikilia bunduki, huyo ni Berta Abelenda Fernandez, "ni miongoni mwa wanawake ambao walitumiwa katika picha nyingi za Ospaaal", Bi Ahmad alieleza.

Haki miliki ya picha Berta Abelénda Fernández
Image caption Siku ya mshikamano kwa watu wa taifa la Guinea-Bissau na Cape Verde, 1968
Haki miliki ya picha Ospaaal
Image caption Picha iliyopo kwenye kasha la jarida la 'Tricontinental' mwaka 1995

Castro alijitoa sana katika taifa la Angola, sio kama kwenye operesheni ya siri ya Cuba barani Afrika ya mwaka 1960s, wakati ambao kulikuwa na fursa nyingi za kujinadi kimataifa kuhusu mshikamano na kuleta mabadiliko kidunia.

Baada ya Angola kupata uhuru wake kutoka kwa wareno mwaka 1975, Castro alituma msaada wa kijeshi kwa kutuma wanajeshi wake 35,000 kusaidia na kusitisha chuki dhidi ya ubaguzi wa rangi huko Afrika kusini , jambo ambalo Marekani lilipanda katika utawala wake.

Haki miliki ya picha José Lucio Martínez Pedro
Image caption Angola, 1972

Inakadiriwa kuwa wacubani wapatao 4,300 waliuwawa katika migogoro ya Afrika, nusu yao waliuwawa nchini Angola peke yake katika mapigano yaliyoisha mwaka 2002.

Picha hizi zinabeba ujumbe wa mshikamano waukombozi .

Picha hizi wameweka maelezo ya lugha nne, kiingereza, kifaransa, kispaniola na kiarabu ili ziweze kuenea katika maeneo mngi zaidi ya Cuba pekee.

Haki miliki ya picha Gladys Acosta Ávila
Image caption Wiki ya kimataifa ya International Week of Solidarity with the Peoples of Africa, 1970

Unaweza kusoma pia:

Haki miliki ya picha Olivio Martínez Viera
Image caption Harakati za watu wa Msumbiji, 1973

Picha nyingi zimelenga mapambano dhidi ya watu wachache weupe nchi Afrika Kusini , mapambano ambayo yaliweza kutokomezwa mwaka 1994, wakati ambapo Nelson Mandela alipochaguliwa kuwa rais.

Haki miliki ya picha Berta Abelénda Fernández
Image caption Afrika kusini , 1968

Kitabu cha mapinduzi ya Cuba Marekani kilitoa fursa ya kuitangaza ndege ya Afrika kusini na kuijumuisha kwenye mkutano wa 'Tricontinental' wa mwezi Julai -Agosti mwaka 1968 ikitoa ahadi ya kutokomeza ubaguzi wa rangi ambao umesababisha kundi kubwa la waafrika waliopinga ubaguzi kuwekwa gerezani na maelfu ya waafrika wakiwa wanafanyishwa kazi kama watumwa katika migodi na maeneo mengine.

Haki miliki ya picha Rafael Morante Boyerizo
Image caption Afrika Kusinia - ubaguzi wa rangi, 1982

Baada ya Mandela kufungwa gerezani mwaka 1964, ilikuwa ni kosa la jinai nchini Afrika kusini kwa mtu kumpiga picha au kuchapisha picha yake ya zamani . Picha ya mchoro huu ilitolewa mwaka 1989, mwaka mmoja kabla hajatolewa gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.

Haki miliki ya picha Alberto Blanco González
Image caption Nelson Mandela, 1989

Msanii aliyechora picha hiyo alikuwa anakaa Havana na alikuwa anajaribu kutumia uwakilishi wa watu kiuhalisia katika siasa.

Haki miliki ya picha Víctor Manuel Navarrete
Image caption Ushindi wa Namibia 1977
Haki miliki ya picha Jesús Forjans Boade
Image caption Ukombozi wa Zimbabwe, 1969

Dhana ya mshikamano kimataifa imebadilika na unaweza kuona ni kwa nini?

Haki miliki ya picha Lázaro Abreu Padrón
Image caption Uhuru wa Zimbabwe, 1980

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii