Vurugu za maandamano Hong Kong yanaendelea
Huwezi kusikiliza tena

Mamia ya waandamanaji wanajaribu kuondoka katika maeneo ya ghasia

Kati ya waandamanaji 100 mpaka 200 bado wapo ndani ya chuo kikuu cha Hong Kong huku polisi wakiwa wameweka doria kwa muda wa siku tatu.

Watu waliopo ndani ya chuo kikuu cha Polytechnic imedaiwa kuwa na uhaba wa mahitaji.

Waandamanaji wamekuwa ndani ya maeneo ya chuo tangu wiki iliyopita, huku wakiwazuia polisi kuingia ndani kwa kuwasha moto na kulipua mabomu ya petroli.

Polisi wanasema kuwa lazima watu wakamatwe, ingawa baadhi wana uoga sana wanataka kuondoka.

Mamia ya waandamanaji walikuwa wanajaribu kukimbia katika maeneo hayo lakini wengi walirusha mabomu ya machozi na kukamatwa.

Mada zinazohusiana