ATM za maziwa yawaomboa wafugaji wa Kilimanjaro.

Maziwa ,kilimanjaro Haki miliki ya picha Eagan Salla BBC
Image caption Maziwa ,kilimanjaro

Nchini Tanzania wengi wao wanaposikia ATM kitu cha kwanza wanachoweza kufikiri huenda ikawa ni chombo cha kutolea fedha.

Jambo ambalo ni tofauti huko Kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro ipo ATM ya kwanza ya maziwa ambayo imeguka kivutio kwa wakazi wa mkoa huo.

Unaweza ukajiuliza ATM hiyo inafanyaje kazi?

Nancy Manase ni wenyekiti wa umoja wa wanawake wa maziwa

''Uone labda tulikuwa tunauza lita mia tatu kwa siku au mia nne sasa tumeongezea lita mia moja juu kwahiyo ni faida na msimu huu ni ule msimu unaokuwa na maziwa mengi sana huku kwetu maziwa yanakuwa mengi mpaka yanamwagwa kwahiyo mpaka sasa hivi hatujamwaga maziwa''.

ATM inatusaidia na watu wamepata elimu kunywa maziwa ni afya kwa sababu hata usipokula kitu kingine inakutosha''

Kila lita moja inagharimu wastani wa dola moja

Lakini katika mashine hii unaweza kununua maziwa ya kiwango chochote kulingana na hela ulionayo

Haki miliki ya picha Eagan Salla BBC
Image caption Maziwa

''Kwa muda mfupi niliokuwa hapa katika ATM hii ya maziwa mkoani Kilimanjaro changamoto kubwa inayo ukabili mradi huu uliotokea kupendwa na walio wengi ni nishati ya umeme iwapo umeme utakatika basi ni vigumu kuipata huduma''

Huwezi kusikiliza tena
Fahamu jinsi ATM ya maziwa inavyofanya kazi

Wafugaji mmoja baada ya mwingine huleta maziwa yao hapa kwa ajili ya vipimo na kuandaliwa tayari kwenda kwenye ATM

Haki miliki ya picha Eagan Salla BBC
Image caption Mashine ya kununulia maziwa

Kwa upande wa wafugaji wanasema wameanza kuyaona matunda ya uwepo wa ATM hizi

Aleningwasa Swai ni mfugaji ambaye ananufaika na huduma hii.

"Maziwa yalikuwa hayana bei yalikuwa yananunuliwa kirojorojo tu, lakini tangu huu mradi ulipoanza wa kupeleka maziwa mjini tumepata faida sana , maziwa yanachukuliwa mwisho wa mwezi unakwenda kuchukua hela yako''.

Kwa wateja wa maziwa kwenye ATM nao walikuwa na maoni yao kuhusu mradi huu

"Maziwa ni mazuri nimeshakunywa maziwa sehemu nyingi, maziwa ya hapa nimeona kuna utofauti kidogo, cha kwanza maziwa yatoka kwenye ATM halafu istoshe maziwa ni mazuri kwa hiyo muda wote mtu ukihitaji maziwa ya kuchemsha na chai unapata muda wowote'', anaeleza mteja wa maziwa, Martin Karata

''Huduma hii ni nzuri ukija kwa muda wowote unapata maziwa, ikiwa asubuhi mchana jioni unapata maziwa,"Neema Munisi ni mteja pia.

Kwa sasa zipo ATM mbili tu kwa mkoa mzima

Na walio wengi wanatamani ziongezwe na kusambaa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu

Kama kwenye vituo vya mabasi, Hospitalini na hata sokoni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii