Fahamu sababu zinazowafanya vijana kuwa na ghadhabu wanaponyimwa simu

Vijana wengi wana uraibu wa simu janja Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vijana wengi wana uraibu wa simu janja

Karibu robo ya vijana wamejenga tabia ya utegemezi wa simu zao na tabia hiyo imekuwa kama uraibu, utafiti umebainisha.

Utafiti uliofanywa katika chuo cha King kilichopo London, unasema kuwa watu wanakuwa na hofu na kukasirishwa kama wakinyimwa mwanya wa kuwa na simu.

Vijana wamekuwa wanashindwa kupanga muda sahihi wa kutumia simu.

Utafiti huu umetoa angalizo kuwa uraibu huu una athari kubwa sana za afya ya akili.

Utafiti uliojumuisha vijana 42,000 umebaini kuwa utumiaji wa simu janja (smartphone) umeweza kuleta madhara makubwa kwa watumiaji.

Tafiti iliweza kubaini 23% walikuwa wana uraibu kuwa hawawezi kukaa muda bila kutumia simu zao, kushindwa kwao kupanga muda wa kutumia simu na kutotumia umesababisha washindwe kufanya kazi zao ipasavyo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Uraibu wa namna hiyo unaweza kuhusishwa na matatizo mengine kama vile msongo wa mawazo, kukosa usingizi na matokeo ya masomo yao kushuka.

"Simu janja zipo na teknolojia yake inaendelea kukua na jamii wanapaswa kuelewa matumizi yake," alisema mtafiti, Nicola Kalk, kutoka chuo hicho cha Uingereza.

"Hatufahamu kama ni simu janja ndio inasababisha uraibu huo au programu zilizopo kwenye simu (app)ndizo zinafanya watu wawe na uraibu," alisema Dr Kalk.

"Ingawa kuna haja ya vijana na watoto kuwa na uelewa mzuri kuhusu simu zao na wazazi wanapaswa kufahamu ni muda gani ambao watoto wanatumia kwenye simu zao."

Muandishi mwingine wa tafiti hiyo bwana Samantha Sohn ameonya kuhusu uraibu huu na kusema kuwa uraibu huu unaweza kusababisha madhara makubwa ya afya ya akili na kuathiri majukumu ya kila siku".

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii