Timothy Weeks anakumbuka alivyoteswa Taliban - 'Sikuwahi kukata tamaa'

Timothy Weeks Haki miliki ya picha EPA
Image caption "Wakati unapokata tamaa, kuna nafasi ndogo ya matumaini kwao"

Mhadhiri wa Australia aliyechiwa huru Taliban kwa kubadilishana na mfungwa amezungumzia kuhusu mateso aliyopata kwa muda mrefu wakati alipokuwa mateka huko Afghanistan.

Timothy Weeks alisema kuwa aliaamini kuwa jeshi la Marekani lilijaribu kutaka kumuokoa mara sita., yeye pamoja na Kevin King ambaye aliachiwa huru pia.

Bwana Weeks anasema kuwa halikuwa hawachukii raia wa Taliban , baadhi ya walinzi walikuwa watu wazuri sana na hata walikumbatiana wakati anaondoka.

"Sikuwahi kukata tamaa... nilijua kuwa ipo siku nitaondoka tu," alisema.

Bwana Weeks na bwana King, ambaye pia alikuwa muhadhiri waliachiwa huru mwezi huu kwa makubaliano ya kubadilishana na wakuu wa jeshi watatu ambao walikuwa wameshikiliwa na mamlaka ya also an Afghan, kwa lengo la kuafikiana kuanza mazungumzo ya amani.

Wahadhiri hao wawili waliwekwa mateka kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kutekwa nje ya chuo kikuu cha Marekani kilichopo Afghanstan mji wa Kabul, eneo ambalo maprofesa hao walikuwa wanafanyia kazi.

Bwana Weeks, mwenye umri wa miaka 50 anayetokea eneo la Wagga Wagga ,New South Wales, alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kurusu kurejea kwake.

Alisema kuwa anaamini uwa kuna majaribio kadhaa yalifanywa ili kuweza kumuokoa katika maeneo ambayo alikuwa amewekwa matekwa huko Afghanistan na Pakistan, ambapo kote jela zake zilikuwa na dirisha dogo sana .

"Ninaamini na ninatumaini kuwa kuwa sawa, kulikuwa na vikosi maalum vya usalama ambavyo vilikuja mara sita kutaka kutuokoa, na mara zote walipokuja walikuwa wanatukosa kwa saa chache tu," Bwana Weeks alisema.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Timothy Weeks akiwa na dada zake, Alyssa Carter (kushoto) na Joanne Carter (kulia)

Anakumbuka shambulio moja lililotoa mwezi April, ambapo walinzi waliokuwa wanamlinda walimwambia kuwa walikuwa wameshambuliwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu yaani IS.

"Niliamini kuwa kuwa wale ni wanajeshi wa 'Navy SEALs' waliokuja kutuokoa ," bwana Weeks alisema.

"Niliamini kuwa walikuwa nje ya mlango wetu. kwa sababu ndio wakati tulikuwa tunapitishwa kwenye njia za chini ya ardhi, maana tulivyokuwa tumeingizwa kwenye vichuguu kama mita mbili tu tunasikia mlango tuliokuemo unabamizwa.

"Na walinzi wetu walikuepo na silaha kali nyingi. Walinisukuma na kujigonga mwenyewe , nikapoteza fahamu"

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Weeks (kushoto) na mateka mwenzie Kevin King

Alisema kuwa alikuwa anakubali kila kitu anachoamrishwa kufanya na askari hao kwa sababu alikuwa hana namna nyingine.

" Siwachukii wote kabisa yaani," alisema. "Baadhi yao nawapa heshima kubwa sana na ninawapenda. Kuna wengine walikuwa wana huruma kweli na walikuwa watu wenye roho nzuri. Na wananifanya niwafikirie...imekuwaje wamefiia kufanya kazi ile ?"

Bwana Weeks alikumbuka pia kuachiwa kwake , alisema kuwa alipoona helikopta mbili zikishuka kutoka angani alianza kuona kama shida zote zimefikia hatima yake.

shida "ilimalizika ghafla kama ilivyokuwa imeanza" wakati helikopta mbili za Nyeusi za Merika zilishuka kutoka angani.

Bwana Weeks alisema kuwa msaada huo alipokuwa mateka ni kitu ambacho hakuwahi kukifikiria kuwa kitatokea.

Licha ya kuwa hakuwahi kukata tamaa kwa sababu anaamini kuwa "Wakati unapokata tamaa, kuna nafasi ndogo ya matumaini kwao"

Alisema pia kuwa kuna wakati alihisi kuwa kifo chake kilikuwa kimekaribia na asingeweza kurudi nyumbani kwa wapendwa wake. Lakini kwa mapenzi ya Mungu sasa yu hai na salama akiwa huru pamoja na familia yake tena.

Soma pia:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii