Vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu Burkina Faso

A close-up shot of an Islamist militant wearing a black veil which only shows his eyes Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanamgambo wa kiislamu wamekuwa wakifanya mashambulizi Sahel lakini sasa wamehamia Burkina Faso

Mashambulio ya makanisa kaskazini mwa Burkina Faso yanadaiwa kufanywa na makundi ya kijihadi ambayo yanazidi kukua katika ukanda huo licha ya uwepo wa operesheni ya kuwakabili.

Waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo alisema kuwa kukabiliana na magaidi imekuwa ni vita ya wale waliosalia katika mji wa Sahel wakishirikiana na Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger.

Mpaka sasa wanamgambo wamewalazimisha wakazi wapatao 100,000 wa Burkina Faso kuhama makazi yao mwaka huu.

Wanamgambo hao ni kina nani?

Makundi ya wapiganaji wa kiislamu ambayo yameshika doria kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso ni Ansarul Islam, Kundi la Kuuunga Mkono Waislamau na Uislamu (GSIM) na Dola ya Kiislamu katika Jangwa la Sahara (ISGS).

Shambulio la kutisha zaidi lililofanywa miaka ya hivi karibuni- lilikuwa mwezi Januari 2016 katika hoteli moja ya kifahari, ambapo watu 30 waliuwawa nchini Burkina Faso katika mji mkuu wa Ouagadougou.

Shambulio hilo lilifanywa na al-Qaeda tawi la Magharibi na Sahara, huku makundi mengine mawili ya kijihadi yakiibuka ni - Ansar Dine na al-Mourabitoun - yanayounda kundi linalofahamika kama GSIM.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabomu yaliyotolipuka kutoka kwenye magari

Makundi hayo yapo Mali, Niger na Burkina Faso. Vilevile yalihusika katika mashambulizi mawili mengine yaliyotokea katika mji wa Ouagadougou, mwezi Agosti mwaka 2017 mgahawa ulishambuliwa na mawezi machi 2018 ubalozi wa Ufaransa na makao makuu ya jeshi.

Video ya kipropaganda ilitolewa mwezi Aprili 2019, na kundi la wanamgambo wa kiislamu (Islamic State-IS) ikimuonyesha Sahel akiwataarifu wafuasi wote wa Jihad duniani kuwa ndugu zao wa Burkina Faso na Mali wanapaswa kupongezwa kwa shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya.

Ansarul Islam, ikimaanisha walinzi wa waislamu ni kundi ambalo lilanzishwa mwaka 2016 na sasa linaonekana kukuwa, mhubiri maarufu Ibrahim Malam Dicko, aliwahi kusema kuwa nani walipiganan na wanamgambo wa kiislamu nchini Mali wakati walipoingia kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2012, na kufukuzwa na wafaransa.

Dicko alifariki mwezi Aprili mwaka 2017 na kaka yake Jafar ambaye anaongoza kundi kwa sasa huku akiungwa mkono na kundi la AQIM na ISGS, kwa mujibu wa Human Rights Watch.

Ukosefu wa ajira imewafanya vijana wengi nchini Burkina Faso kujiunga na makundi ya kijihadi na kubadili mtazamo wao wa kiislamu.

Kwa mujibu wa wachumi, migogoro mingi kati ya wakulima na wafugaji au dhidi ya utawala wenye rushwa ndio imepelekea wengi kujiunga na wana Jihad kwa sababu wao ni waislamu.

Kwa nini makanisa ndio yanalengwa zaidi?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Burkina Faso ina historia ndefu ya mivutano ya kidini: Picha hiyo Askofu wa Ouagadougou Philippe Ouedrago (kushoto) akiwa anamtakia heri ya Iddi chifu Mogho Naba Baongo nchini Burkina Faso, 2012

Mwezi Aprili mwaka 2019, mashambulio matano yalikuwa yamelenga wakristo katika ibada mbalimbali kanisani.

Makundi ya kijihadi yalisema kuwa yanahusika na mashambulizi hayo na wachambuzi pia walisema kuwa mashambulizi hayo yaliacha ishara kuwa ni wana jihad ndio walihusika.

Mtaalamu

"Mara nyingi wakristo ambao ni wachache wamekuwa wakikabiliana na vurugu ambayo ilikuwa inafanywa na wana jihad tangu waingie katika eneo hilo".

Mgogoro huu kati ya wakristo ambao ni wachache kushambuliwa na wanajihadi imekuwa ikisababisha Burkina Faso kuwa na historia ya muda mrefu ya uvumilivu wa kidini.

Mizozo hiyo ikiwa sehemu ya mikakati ya wanajihadi waliyoiweka.

Ukosefu wa amani na migogoro imefanya wana jihadi kuweza kutawala eneo hilo.

Namna gani wana Jihad wameweza kuathiri maisha ya watu?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanamgambo wa kijihadi

"Usalama wa taifa hilo umeshuka kila siku," alisema bwana Audet-Gosselin. "makundi ya kijihadi inaongeza umaarufu katika maeneo kadhaa."

Shule na walimu wamelengwa zaidi na kundi la wanamgambo wa kiislamu la IS ambao walikuwa wanapinga mfumo wa elimu.

Zaidi ya shule 1,000 kaskazini mwa nchi hiyo zililazimika kufunwa na kuathiri elimu ya watoto 150,000.

Mashambulio yaliyotokea hivi karibuni Burkina Faso

 • 31 Decemba 2018: Watu saba waliuliwa na watu waliodhaniwa kuwa wana Jihadi katika eneo la Yirgou, jumuiya ya wakulima.
 • 01 Januari 2019: Wanakijiji wa Yirgou na baadae shambulio la wafulani katika eneo hilo na watu 39 kuuwawa.
 • 17 Januari: Jiolojia raia wa Canada alikutwa amekufa baada ya kutekwa mgodini.
 • 20 Machi: Walimu wawili walitekwa katika shule waliokiuwa wanafundisha katika mji wa Djibo na kuuwawa - serikali wanasema watekaji walitaka kuwatisha walimu ili waache kazi ya ualimu katika eneo hilo
 • 03 Aprili: Shambulio ambalo liliuwa watu karibu saba kaskazini mwa mji wa Arbinda, na kusababisha vurugu ya wenyewe kwa wenyewe ambao uisababisha watu 62 kuuwawa kwa mujibu wa serikali.
 • 05 Aprili: watu wanne waliuwawa wakati ambao kanisa katoliki liliposhambuliwa katika kijiji cha jirani ambacho askofu wa Dori wa kaskazini mwa Burkina Faso
 • 28 April: Mchungaji na watu watano waliuwawa katika kanisa la kiprotestanti lililopo Silgadji, kaskazini mwa taifa hilo.
 • 11 Mei:Raia wa kigeni wanne kutoka Ufaransa, Marekani na Korea waliowekwa mateka Burkina Faso na kuachiwa, lakini muongoza watalii na askari wawili wa ufaransa waliuliwa wakati wakati wa harakati za uokoaji.
 • 12 Mei: Wanaume wenye silaha waliwauwa watu sita ambao walikuwa wakisali kanisani , padre akiwemo katika kanisa la Dablo kabla ya jengo la kanisa hilo kubomolewa.
 • 13 Mei: Wakatoliki wanne waliokuwa wanatoa heshima kwa bikira maria waliuwawa na wanaume wenye silaha katika mji wa Zimtenga, kaskazini mwa nchi hiyo.
 • 26 Mei: Watu wenye silaha waliwauwa wakatoliki waliokuwa kwenye misa ya jumapili lioenda katika mji wa ToulfĂ©.
 • 01Desemba: Watu 14 wameuwawa katika la shambulio lililotokea kanisani

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii